The House of Favourite Newspapers

Idahams Aachia Man On Fire X Falz, Peruzzi, Seyi Shay

0

MSANII anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Nigeria, Idahams amefanikiwa kukivuka kikwazo cha maradhi ya Covid-19 kwa kuachia albamu maalum (Extended Play- EP) iitwayo ‘Man On Fire’ yenye jumla ya nyimbo saba zilizobeba ujumbe wa kuwafariji na kuwapa moyo watu wote katika kipindi hiki kigumu ambacho dunia inapambana na Janga la Corona.

 

Nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za muziki ikiwemo Afro Pop, Rap na aina nyingine hususan unaopatikana barani Afrika, ukiwemo wimbo wa Ada na Man on Fire alizoshirikiana na mwanamuziki mwingine, Falz, Shima alioshirikiana na Peruzzi na Seyi Shay.

Katika albamu hiyo, Idahams anaendeleza moto aliouwasha mwaka 2020 kwa kutoa nyimbo kali zaidi ya zile zilizopo kwenye albamu yake iliyopita kama Belle, God When na No One Else alioutoa mwaka 2018 ambao ulisababisha asainiwe na lebo kubwa za Universal Music na Grafton Records.

 

Katika albamu hiyo, Idaham ameendelea kuonesha uwezo mkubwa wa namna anavyoweza kutunga nyimbo zenye mashairi mazito, zilizoandaliwa na maprodyuza bora kwa kuzingatia asili yake ya Kusini mwa Nigeria sambamba na midundo mizuri inayomfanya kuendelea kuwa msanii tishio barani Afrika.

Na Mwandishi Wetu

 

Leave A Reply