The House of Favourite Newspapers

LIVE: IBADA IJUMAA KUU KITAIFA YAFANYIKA KKKT LUKAJANGE, KARAGWE

WAKRISTO nchini leo wameungana na wenzao  duniani katika kuadhimisha ibada ya Misa Takatifu ya Ijumaa Kuu, siku ambayo kiongozi wao, ambapo ibada kuu kitaifa imefanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushariki wa Lukajange, Karagwe, Mkoani Kagera.

 

Ibada hiyo ni katika kuadhimisha mateso ya Yesu Kristo, aliyeteswa hadi kufa msalabani kwa ajili ya kuwaokoa watu wote wanaoamini katika Ukristo.

 

Kwa mujibu wa imani yao, Yesu Kristo alipaswa kuteswa na kuuawa msalabani ili kuwakomboa binadamu kutoka katika dhambi na hatimaye kumrudia Mungu, kwa kuwa hiyo ndiyo kazi pekee iliyomleta duniani.

 

Kufuatana na taarifa za Injili nne katika Biblia,  Yesu alisulubiwa siku kabla ya Sabato (Jumamosi), yaani Ijumaa, katika mlima wa Golgotha nje ya ukuta wa mji wa Yerusalemu.

Comments are closed.