The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awaapisha Viongozi Aliyowateua – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha viongozi wateule wafuatao:-

1. Prof. Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

2. Balozi Mteule Lt. Jen. Yakub Hassan Mohamed kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki.

3. Balozi Mteule Mahmoud Thabit Kombo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

4. Balozi Mteule Elsie Sia Kanza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

 

“Nianze na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, mengi yalishasemwa. Una kazi ya kuhakikisha magereza hayajai watu wasio na makosa kwamba haki inatendeka. Pili unapaswa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira mazuri na maslahi yao.

 

“Tuko kwenye maboresho makubwa ya Mahakama, tunajenga na kukarabati majengo ya Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi, za wilaya na zile za mwanzo. Pia tuko kwenye majaribio ya Mahakama zinazotembea na zinafanya vizuri hapa Dar.

 

“Pengine wengi wanaweza kushangaa kwanini Maasai ametolewa kwenye ng’ombe na kupelekwa kwenye Mahakama (Mtendaji Mkuu wa Mahakama), lakini najua unaweza kufanya vizuri eneo hilo. Kwahiyo achana na ng’ombe kwa sasa nenda kawatumikie watu.

 

“Kwa mabalozi wapya, nakumbuka 27 Julai niliwaeleza wenzenu kwamba jukumu namba moja kwetu ni kuendeleza Diplomasia ya Uchumi ingawa tutakwenda kuipitia sera yetu na kuongeza mengine ambayo kwa wakati huu tutayafanyia kazi.

 

“Yapo baadhi ya mambo mahsusi ambayo natamanai mkayafanyie kazi, nianze na Balozi wa Marekani nimekutoa World Bank bila kukushauri. Nimeona kazi nzuri unayofanya nikajua kwa nchi yetu ilivyo sasa na nchi ya Marekani wewe ungetufaa pale.

 

“Balozi wetu Italia unatuwakilisha katika kwenye mashirika ya Kimataifa, WFP, FAO na IFAT kwahiyo huna budi kuendeleza mashirikiano mazuri. Mfano WFP ni wanunuzi wazuri wa mahindi yetu, ni vizuri uwashawishi wanunue mahindi zaidi,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply