The House of Favourite Newspapers

Makamanda wa Majeshi Kuingia Mazoezini Siku 17 Kupambana na Ugaidi, Maafa (VIDEO)

Brigedia Kapinga.

MAJESHI yaliyoko ndani ya nchi tano zinazounda Umoja wa Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi yanatarajia kuanza mazoezi maalum kwa ajiri ya kuongeza ujuzi, mbinu na maarifa zaidi katika kupambana na ugaidi, maafa na oparesheni nyingine za ulinzi na usalama.

 

Akizungumza na wanahabri jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Desemba 4 hadi 20, 2017, Mkuu wa Tawi la Utendaji Kivita na Mafunzo Jeshini, Brigedia Jenerali Alfred Fabian Kapinga alisema mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku 17 kuanzia Desemba katika kituo Maalum cha Mafunzo kilichopo, Kunduchi Dar, ambapo washiriki watakuwa ni Jeshi la Ulinzi Tanzania, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu wa Maafa, Kituo cha Taifa cha Kupambana na Ugaidi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi.

 

Kapinga amesema maudhui ya mazoezi hayo yamejikita katika maeneo manne ambayo ni; Oparesheni za Ulinzi wa Amani, Kupambana na Ugaidi, Kupambana na Uharamia hasa katika bahari na Kupambana na Majanga kama moto na mengine. Aidha Kapinga amesema mambo yote hayo yanapaswa kutatuliwa kwa kutumia uzoefu ambao makamanda hao wataupata.

VIDEO: MSIKIE MEJA JENERALI KAPINGA AKIZUNGUMZA

Comments are closed.