The House of Favourite Newspapers

VIDEO: JPM ATEMBELEA UJENZI WA MELI MPYA MWANZA SOUTH

Rais John Magufuli leo Julai 16, 2019, amefanya ziara katika bandari ya Mwanza South kukagua ukarabati wa meli mbili zinazoendelea kutengenezwa, MV Victoria na MV Butiama ambazo zitakamilika mwezi wa tatu mwakani.
Pia ameelezwa kuwa injini mbili mpya za MV Victoria na jenereta tatu zitakuwa zimewasili nchini mwezi wa tisa mwaka huu.

akiongea na Wafanyakazi wa bandari ya Mwanza South wamemwambia kuwa hawalipwi pesa zao vizuri na akatumia muda huo kumtaka kiongozi wa TPA kujibu maswali.

“Huyu wa TPA yupo wapi?  Njoo hapa, haya jibu haya maswali kwa nini hamuwalipi mishahara vizuri? Mnawabebesha mizigo mingi mpaka huyu baba ameshindwa kununua viatu vizuri na suruali yake ina viraka kwa sababu hamumlipi vizuri na kazi anafanya,  mikono na kiuno vyote vimeumia.  Mna mpango gani wa kuangalia maslahi ya hawa watu?” – Rais Magufuli

 

Comments are closed.