The House of Favourite Newspapers

Live Kutoka Ikulu Dar… Ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia

IKULU DAR: Kufuatia Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn kuwasili hapa nchini kwa ziara ya siku mbili, serikali ya Tanzania na ya Ethiopia zimesaini Mikataba mitatu ambayo ni;

  1. Mkakati wa Ushirikaiano wa Kati ya Serikali hizo mbili.
  2. Mkataba wa Ushirikiano wa Kupambana na Uhamiaji, Afya na Teknolojia kati ya nchi hizo mbili.
  3. Hati ya Makubaliano Katika Sekta ya Utalii kati ya nchi hizo mbili.

Baada ya Mikataba hiyo kusainiwa, Rais Magufuli ameyasema haya;

“Tumekubaliana mambo 15 ikiwemo ushirikiano wa mashirika yetu ya ndege, wao wana ndege nyingi Afrika na nje.

“Tumekubaliana kujenga cargo hapa Dar, ambayo itakuwa kubwa Afrika yote.

“Tumekubaliana watatusaidia training na matengenezo ya ndege zetu.

“Tumekubaliana suala la Umeme kutoka Ethiopia ambao watatuuzia kwa bei ndogo kwani wao wanasupply hadi Kenya

“Tumekubaliana kuhusu Visa ambazo hapo mwazo zilikuwa vikwazo kwa biashara baina ya Watanzania na Ethiopia.

“Waziri Mkuu amekubali kufungua ubalozi Dodoma, nimekubali kumpa eneo la kujenga ubalozi na makazi.

“Waziri Mkuu amekubali kuchagua chuo kikuu nchini kwake kifundishe Kiswahili, tutampa maprofesa wafundishe huko.

“Pia tuitashirikinana kuendeleza utalii, na ushirikiano katika majeshi.” Alisema Rais Magufuli.

TAZAMA TUKIO LOTE LILIVYOKUWA

Comments are closed.