The House of Favourite Newspapers

LIVE: Kutoka PUGU, MAITI Iliyofukuliwa na Kuachwa Utupu, Yadaiwa Kubakwa – Video

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa aliyekuwa Ofisa wa Wizara ya Madini, MERY MKWAYA MALAMO, aliyefariki mwanzoni mwa wiki hii na kuzikwa jana katika makaburi ya Pugu-Mwakanga jijini Dar es Salaam, umefukuliwa na kutolewa nje ya jeneza kisha kuvuliwa nguo usiku wa kuamkia leo, Ijumaa, Aprili 12, 2019 na watu wasiojulikana.

 

Global TV Online na Global Publishers wamefika neo la tukio katika makaburi hayo na kujionea hali halisi ilivyokuwa ikiwa ni pamoja na kuzungumza na fundi aliyejnga kaburi hilo aitwaye Andrew Bethlehem Butta ambaye ndiye wa kwanza kushuhudia tukio hilo.

 

Butta anadai alifika katika makaburi hayo leo asubuhi kwa ajili ya kumwagilia kaburi na kutoa mbao za zege kama alivyokuwa amkubaliana na familia ya marhemu.

 

Anadai, alipofika katika kaburi kwa mbali aliona nguo nyeupe, aliposogea kuchungulia ndipo akabaini kaburi lilikuwa limebomolewa na mwili wa Mery ukia umevuliwa nguo zote na kubakizwa mtupu huku mguu mmoja ukiwa umetanulia hali ambayo ni udhalilishaji jambo lililomshtua na kuwajulisha viongozi wa Srikali na familia ya marehemu.

 

Mbali na fundi huyo, Mwenyekiti wa shina ambapo makaburi hayo yapo, Bi. Rose ambaye amesema tukio kama hilo halijawahi kutokea katika amakaburi hayo ndiyo mara ya kanza, baada ya kupewa taarifa na fundi Andrew aliamua kumjulisha menyekiti wa Mtaa ambaye aliwajulisha polisi na ndugu.

 

Baada ya kufika eneo hilo walifanya uchunguzi kutokana na hali walivyoikuta maiti hiyo huku ikidaiwa huenda maiti ilibakwa lakini haijathibitishwa kwa sababu uchunguzi bado unaendelea, ndipo wakakubaliana mili uzikwe na kaburi kujengelea upya.

 

Aidha, wananchi na viongozi wa eneo hilo wameiomba serikali kushirikiana na wamiliki wa eneo la makaburi hayo ambao ni wamisionari kuweka uzio,walinzi na kibanda cha ulinzi ili kuhakikisha amani katika makaburi hayo.

FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.