The House of Favourite Newspapers

PAPA FRANCIS ABUSU MIGUU YA KIIR NA MACHAR

KIONGOZI  wa kanisa Katoliki dunian,i Papa Francis, amefanya tendo la unyenyekevu na ambalo halikutarajiwa baada ya kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini, akiwahamasisha kuuendeleza mchakato wa amani.

 

Mwishoni mwa ziara ya kiroho ya siku mbili ya viongozi hao wa Afrika mjini Vatican, Papa Francis alimuomba Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir,   na hasimu wake, Rieck Machar, kuendeleza mazungumzo ya amani licha ya kuongezeka kwa ugumu, na kisha alipiga magoti na kubusu miguu yao, pamoja na ya Makamu wa Raism Rebecca Nyendeng Garang.

 

Papa  hufanya tendo la kitamaduni la kiimani la kuwaosha miguu wafungwa siku ya Alhamisi Kuu, lakini hajawahi kufanya tendo kama hili kwa viongozi wa kisiasa.

 

Alisema mwishoni mwa ziara hiyo kwamba anatarajia kusitishwa kwa uadui, mapigano, mgawanyiko wa kikabila na kurejeshwa kwa hali ya amani nchini humo.

 

Comments are closed.