The House of Favourite Newspapers

CUF ya Lipumba Yamlipua Mtulia, Yaanika Alichokifanya Kabla ya Kuhamia CCM -(VIDEO)

CHAMA cha Wananchi upande wa Prof. Ibrahim Lipumba, leo Desemba 4, 2017 kimetoa ufafanuzi huu aliekuwa Mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia aliyejivua uanachama na kuachia ngazi nyadhifa zote ndani ya chama hicho huku akitangaza kuhamia CCM.

CUF imefunguka leo ikiwa ni siku moja tangu Mtulia atangaze uamuzi huo juzi ambapo alisema ameridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli hivyo haoni haja ya kuendelea kuwa mpinzani hivyo ni bora akamuunga mkono Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF, Abdul Kambaya amesema kuwa Maulid Mtulia ameondoa uaminifu kwa wanachama wa Jimbo la Kinondoni kwa madai ya kuwa wananchi walimwamini kulala nje wakipigania kula zake za ubunge huku wengine wakiumizwa na kufikishwa mahakamani lakini yeye amewasaliti.

Amesema kuwa Mtulia amekitia doa chama chao kutokana na matande yake aliyoyafanya kwa wananchi na chama kwa ujumla huku akisema kuwa kuhama kwake chama kwa madai yakuwa nikutokana na kwamba anamuunga mkono Rais hazina mashiko hata kidogo.

“Mtulia aliwania udiwani wa Kata ya Ndugumbi mwaka 2005 akashinda kura za maoni lakini baadaye akajitoa, ikabidi niingie mwenyewe kugombea ili niokoe jahazi, mwaka 2015 alijaza vibaya fomu ya kugombea ubunge, akaondolewa na kwenye mchakato, tulipambana hadi akarudishwa na Tume ya Uchaguzi ili ahgombee, hii yote inaonyesha namna gani alikuwa amejiweka sokoni mwenyewe.

“Hoja ya kusema anamuunga mkono Rais Magufuli haina mashiko, alichokifanya Maulid ni kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi na sio Rais, kama amemuunga mkono Rais Magufuli, siku kiongozi huyo akimaliza muda wake atarudi tena CUF?” alihoji Kambaya.

 

Comments are closed.