The House of Favourite Newspapers

Magufuli Ajiuzulu Uenyekiti wa CCM, Agombea Tena – Video

Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli amejiuzulu nafasi hiyo kulingana na katiba ya chama hicho ili kupisha mchakato wa kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho.

 

Magufuli amejiuzulu leo Desemba 18 kufuatia jina lake kupendekezwa kuwania tena kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaofanyika leo mjini Dodoma. Mbali na Magufuli wengine waliojiuzulu ni makamu wenyeviti kwa upande wa Bara na Zanzibar pamoja kamati yake.

“Ndugu wajumbe nimekuwa mwenyekiti wa kikao hiki, na sasa hivi saa tisa kasoro ishirini, Mimi ndugu John Joseph Magufuli na makamu wangu wawili tumejiuzulu rasmi,” alisema Magufuli.

 

Hatua hiyo imekuja baada ya katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana kutaja kipengele cha katiba ya chama hicho kinachomtaka Mwenyekiti aliyeko madarakani kuachia nafasi hiyo endapo amependekezwa kuwania kiti hicho tena. Baada ya hapo, mwenyekiti wa muda aliyependekezwa ni Rais Mstaafu, Benjamin W. Mkapa ambaye ataendesha mchakato mzima wa uchaguzi hadi kuwapata viongozi wa kitaifa wa CCM.

 

“Kanuni zetu zinatutaka baada ya uteuzi huo kutamkwa, mwenyekiti wa chama cha mapinduzi atatamka rasmi kujiuzulu yeye mwenyewe na makamu wake wawili na halmashauri kuu ya Taifa,” alisema Kinana

 

Waliopendekezwa kuwania uenyekiti ni Dkt. John Pombe Magufuli (Tanzania Bara), Dkt. Ally Mohammed Shein (Zanzibar) na Makamu Mwenyekiti Philip Japhet Mangula ambapo kura zimepigwa.

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HILO

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M

Comments are closed.