The House of Favourite Newspapers

Maxcom Yazindua Mfumo wa Malipo Kielektroniki Hospitali ya Muhimbili

0

KAMPUNI ya Maxcom imefanya uzinduzi wa Mfumo wa malipo ya Kielektroniki utakaotumika katika Hospitali ya Muhimbili. Mfumo huo, utapokea malipo kwa njia mbalimbali ikiwemo: Njia ya kadi na malipo kwa kutumia simu.

Mkurugenzi wa Maxcom Afrika, James Onekasati amesema kuwa, wamefanya hivyo kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma, ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa mfumo wenye ubunifu mwingi ili kurahisisha kuwafikia watu wengi zaidi.

Katika utoaji wa zabuni, James ameeleza kuwa walitumia misingi na vigezo vyote. Walitaka mtoa huduma aweke mfumo utakaopokea taarifa mbalimbali za wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali. Jambo ambalo limefanyika.

Alizidi kueleza kwamba, mfumo huo walianza kuupima tangu Julai 2017 na wameona  umekamilika na unafanya kazi kwa ufanisi.

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Kuona zaidi kilichojiri katika uzinduzi huo, tafadhari tazama video hii…

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILI

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Mawakili Kanda ya Ziwa Waliamsha Dude kwa Lissu

 

Leave A Reply