The House of Favourite Newspapers

Mbowe: Hatutasusia Uchaguzi – Video

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hawatasusia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 na kuwataka viongozi, wanachama na Watanzania kuhamasishana kujiandikisha.

 

“Tunatoa rai kwa Watanzania, tusisusie uchaguzi huu wenzetu wa upande wa pili wanatamani tususie. Kwa hizi siku 3 zilizoongezwa, viongozi wetu wa ngazi zote wahamishane watoke kwa maelfu wakajiandikishe, tukisusa tutakuwa tumesusia maisha yetu kwa miaka mitano.

 

 

“Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatupatia watu wanaosimamia maisha ya kila siku ya wananchi, mifumo ya huduma za kijamii na ndiyo Ikulu za wananchi. Ukizuia siasa matokeo yake utapata viongozi ambao hawana uhalali wa kuwaongoza wananchi kwa miaka mitamo ijayo,” amesema Freeman Mbowe.
MSIKIE MBOWE

Comments are closed.