Video: Miss Ustawi wa Jamii, 2017 Kwenye Ukumbi wa King Solomon, Dar

KINYANG’ANYIRO cha kumtafuta Miss Ustawi wa Jamii, 2017 muda huu kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini hapa huku msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol, Mgogosi na wengine kibao wataporomosha burudani ya ukweli.

AKizungumza na Global TV Online matroni na mwalimu wa warembo hao, Catherine Boniphace amesema kuwa warembo wamejipanga vyema kuchuana pia msanii Ben Pol, Mgogosi na wengineo wamedhamiria kukonga vyema nyoyo za wahudhuriaji.

“Mwaka huu tumejipanga kupata mrembo bora na mwenye uwezo wa kuwakilisha vyema mashindano mengine. Tunashukuru Gazeti la Amani linalotoka kila Alhamisi kwa kuwa mdhamini wa Shindano la Miss Ustawi wa Jamii, 2017 linalohusisha warembo 12 kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii kilichopo Kijitonyama jijini hapa,” alisema.


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment