The House of Favourite Newspapers

FT: NJOMBE MJI 0-2 SIMBA KUTOKA SABASABA NJOMBE

NJOMBE MJI v SIMBA SC FT: John Bocco anaunyamazisha Mji wa Njombe, na kuipa Simba SC pointi 3 muhimu. Simba inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 3 kwa kufikisha pointi 49 huku Yanga SC wakifuatia kwa pointi 46.

Dak ya 88, Matokeo bado ni 0-2, mechi inaendelea na dakika zinaelekea mwisho

Dak ya 84, Mpira umesimama tena, Kwasi yuko chini, tayari ushaanza
Dak ya 83, Njombe wanarusha kuelekea lango la Simba, karibu na eneo la goli, rushwa huku mpira unamkuta Mustafa, anapiga shuti kali, mpira unakwenda nje
Dak ya 81, Kichuya anatoka kumpisha Haruna Niyonzima

Dak ya 66, Hatari nyingine kwenye lango la Njombe, kipa anadaka
Dak ya 64, Boccooooo, anaifungia Simba bao la pili kufuatia kazi nzuri ya Shomari Kapombe

Dak ya 59, Mpira umesimama tena, Kotei ameumia
Dak ya 59, Hatari katika lango la Simba, Njombe wanakosa tena nafasi nyingine ya kupata bao
Dak ya 57, James Kotei anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi, mpira umesimama
Dak ya 55, Kocha Masoud Djuma amesimama kuhamasisha wachezaji wake wazidi kupambana

Dak 56, Simba wanaendelea kushambulia timu ya Njombe Mji kwa kasi

Dak 50, Kichuya anakosa bao mabeki wa Njombe wanaokoa mpira huo

Dak ya 49, Bado Matokeo ni Simba 1-0 Njombe Mji

Kipindi cha pili kimeanza na tayari timu zote zinacheza kwa kushambuliana

HALF TIME

Dak ya 45,Dakika zimeongezwa 3 za ziada

Dak ya 42, Nchiiimbi, hatari, namna gani pale mpira umempita mguuni na kukosa kuipatia Njombe bao la kusawazisha

Dak ya 41, Simba wako katikati mwa Uwanja, Kichuya anampasia Okwi, kwake Bocco lakini Mlinzi wa Njombe anamuwahi

Dak ya 39, Mpira umesimama kwa muda, Manula anapewa huduma ya kwanza

Dak ya 38, Njombe wameamka zaidi wakitafuta bao la kusawazisha, wakati huo huo Manula ameumia

Dak ya 37, Njombe wanacheza faulo, piga mbele kabisa kule, Kwasi anaokoa

Dak 37, Mpira umetoka, unarushwa kuelekea Simba

Dak ya 36, Goli Kiki, mpira unapigwa kuelekea Simba

Dak ya 35, Hali ya hewa ya njombe ni baridi muda ni saa kumi na dakika 35 ila inaweza fikiri kama

ni saa kumi na mbili jion

Dak ya 34, Mchezaji mmoja wa Njombe yupo chini, mpira umesimama

Dak ya 33, Njombe wanajitahada kupenya ngome ya Simba wanapopata nafasi lakini inakuwa vigumu kutokana na uimara wa beki ya Simba

Dak ya 28, Bocco sasa anaenda na mpira, anaparamiana na kipa wa Njombe, Mwamuzi anasema mpira uendelee, goli kiki

Dak ya 28, Tayari faulo ishapigwa na inaokolewa na mabeki wa Njombe, pigwa kuelekea langoni mwa Simba, na Manula anaanzisha upya

Dak ya 27, Mpira anao Manula sasa, pasia kwake Gyan, faulo, inapigwa kuelekea Njombe

Dak ya 25, Njombe wamefanya shambulizi moja kwa kupiga shuti kali lakini linakwenda nje, Simba wanaanza

Dak ya 24, Unarushwa tena kuelekezwa Simba, rusha pale unamkuta Okwi, kwake Nyoni, anajaribu kumtafuta Kapombe lakini unatoka nje

Dak ya 22,Umakini wa kichuya unaikosesha simba goli la pili

Dak ya 21,Njombe wanapata nafasi na wanashindwa kuitumia

Dak ya 18, GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO John Bocco

Dak ya 17, Okwi anapamba kutaka kufunga ila mabeki wa njombe mji wanasimama imara kumzuia

Dak ya 14, Simba wanapata kona na njombe wanaokoa

Dak ya 3, Simba wameonekana kuanza kwa kasi dakika hizi za mwanzo wakijaribu kusaka goli la mapema

Dak ya 2,Namna gani Okwi anakosa nafasi ya kufunga bao la mapema. Alipata nafasi akiwa yeye na golikipa

Dak ya 1, Mpira umeshaanza Uwanja wa Sabasaba

Comments are closed.