The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ashiriki Utiaji Saini Mkataba Wa Ujenzi Wa Reli Ya Kisasa (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III). wa kwanza, hafla hiyo imefanyika leo tarehe 28 Desemba 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshuhudia Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora km 368 katika kipande cha tatu cha Ujenzi huo mkubwa wa Reli kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza km 1596 leo tarehe 28 Desemba, 2021, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya Rais Samia, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema mkataba huo unahusisha ujenzi wa reli ya SGR kipande cha kuanzia Makutopora hadi Tabora chenye urefu wa kilomita 368 kwa gharama ya dola bilioni 1.98 ambazo ni sawa na shilingi trilioni 4.4 na ujenzi huo utachukua miezi 46.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji Saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika kipande cha tatu cha mradi huo (Lot III). Wa kwanza (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini (TRC) Bw. Masanja Kadogosa akiweka saini moja ya Kitabu cha Mkataba huo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Desemba 2021.

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli nchini Bw. Masanja Kadogosa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki Bw. Erdem Arioglu wakibadilishana Vitabu vya Mkataba wa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha kutoka Makutupora (Singida) hadi Tabora chenye urefu wa Kilometa 368 katika awamu ya tatu ya mradi huo (Lot III).

PICHA NA IKULU

 

Leave A Reply