The House of Favourite Newspapers

Biashara Kufanyika kwa Saa 24 Kariakoo – Video

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kushikamana na kufanya kazi kwani ninwajibu wa Viongozi hao kufanya kazi kwa niaba ya wananchi kwani wanauwezo wa kuleta mabadiliko makubwa Katika Mkoa huo.

 

Makonda amesema hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa RCC jijini Dar na kuwaasa viongozi wa kisiasa kuwa uchaguzi ujao uwe wa amani kuliko miaka yote.

 

Aidha, Makonda amesema Soko Kuu la Kariakoo sasa litaanza kutoa huduma zake saa 24. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mesema uzinduzi kwa soko hilo kuanza kufanya kazi masaa 24 utafanyika pindi mwezi wa Ramadhani utakapoanza mapema mwaka huu 2020.

 

Pia, Makonda, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuichungunguza Kampuni inayochukua mapato ya faini za maroli na kulipa fedha zote ilizokusanya tangu mwaka juzi.

 

 

“Wanaotukana kwenye mitandao Facebook, Twitter ni matatizo ya lishe duni hivyo tuwasamehe tu. Ukiona mtu anapinga kila kitu kinachofanywa na Rais Magufuli anamatatizo ya lishe ya siku 1000.

 

“Mnazunguka huko duniania, mnaenda ulaya mnacheka cheka mnapewa na vitiketi vya uwongo unakuja hapa mnakuja kutuka maendeleo ya nchi, baadhi ya mataifa mengi yaliyokuwa yakiendelea yameuwawa na neno Demokrasia,” amesema Makonda.

.

Leave A Reply