The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya kiba yafufukia kwa dada’ke!

0

DAR: Unakumbuka lile sakata la kuvunjika kwa ndoa ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na mkewe, Amina Khaleef? Basi sakata hilo limefufuliwa na dada wa jamaa huyo, Zabibu Kiba.  Zabibu amevunja ukimya kuwa, kwa sasa ni kicheko tu. Kabla ya habari hii njema kutoka kwa Zabibu, kulikuwa na madai mengi mitandaoni kwamba ndoa hiyo imeota mbawa kabla ya hivi karibuni wawili hao kuonekana wakiwa pamoja wakati mtoto wao Keenan akitimiza umri wa mwaka mmoja.

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Zabibu alisema kuwa anawashangaa kinoma watu walivyomuona kaka yake na mkewe huyo, wakaanza kusema kuwa kumbe hawajaachana. “Jamani kwa nini watu wanapenda sana kushangilia mahusiano ya watu yakivunjika? Au ndiyo furaha yao? “Ukweli ni kwamba, kaka yangu hajaachana na mkewe. Kama ni matatizo, yapo kwa kila familia.

“Kingine ninampenda sana wifi yangu (Amina),” alisema Zabibu. Zabibu ni mke wa mchezaji wa kulipwa wa Tanzania anayekipiga Klabu ya Highland Park inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Abdi Banda.

Zabibu alisema kwenye ndoa hakukosekani changamoto, lakini kikubwa ni kuzikabili na maisha yaendelee. “Mimi ninawaombea sana siku zote wadumu miaka mingi zaidi maana changamoto zipo siku zote. Cha msingi ni kukaa chini na kuyamaliza kisha maisha yaendelee,” alisema Zabibu.

Mwaka jana kuliibuka tetesi nyingi mitandaoni juu ya kuvunjika kwa ndoa ya Kiba, lakini sasa mambo yametulia, wawili hao wanaendelea na maisha wakiwa wamejaaliwa mtoto huyo mmoja wa kiume.

 

 Stori: IMELDA MTEMA, WIKIENDA

Leave A Reply