The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapigwa na Pyramids FC Kirumba 2-1

YANGA ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa na kazi ya kupindua meza mbele ya wapinzani wao Pyramids FC nchini Misri kwenye mchezo wa marudio utakaopigwa baada ya wiki mbili.

 

Ushindi wa mabao 2-1 walioupata wapinzani wao umeongeza uzito kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa leo uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo wa leo Oktoba 27 ulioanza kwa kasi, Yanga ilikubali kwenda mapumziko ikiwa imefungwa bao 1-0.

Kipindi cha pili walianza kwa kasi bado mambo yalikuwa magumu kwa Yanga na kuwapa nafasi wapinzani wao kuandika bao la pili.

 

Mabadiliko ya kumtoa Mrisho Ngassa nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke pamoja na Juma Balinya kuingia akichukua nafasi ya Makame yaliongeza nguvu kwa Yanga.

Iliwachukua Yanga dakika 90 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Papy Tshishimbi kwa shuti kali akimalizia pasi ya Kaseke.

 

Ili kusonga mbele Yanga itatakiwa kushinda mabao 2 ugenini na wanatakiwa kulinda lango lao lisitikiswe na wapinzani.

Itamkosa bekikisiki, Kelvin Yondan ambaye ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na kadi mbili za njano.

Dakika ya 90+4 Juma Abdul alipiga faulo iliyomkuta All akapaisha
Dakika ya 90+2 yondani anaonyeshwa kadi ya njano ya pili na kupewa nyekundu
Dakika za nyongeza 5

Dakika 90 zimekamilika
Dakika ya 87 Tshishimbi anaandika bao la kwanza akimalizia pasi ya Deus Kaseke

Dakika ya 86 Patrick Sibomana anaingia akichukua nafasi ya Makame
Dakika ya 87 wanaanza kona fupi, Shikalo anaokoa
Dakika ya 86 mpira unasimama kwa muda
Dakika ya 82 Johe Atwi anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Al

Dakika ya 54 Abubakari anarusha mpira vibaya, Sadney anachezewa rafu
Dakika ya 52 kadi ya njano kwa Ahmed Mansour wa Pyramids

Kipindi cha pili kimeanza

Mapumziko
Yanga 0-1 Pyramids Zimeongezwa dakika mbili

Dakika ya 42 Waarabu wanafunga goal
Dakika ya 41 waarabu wanaanzisha mashambuliziDakika ya 40 Ngassa anatoa mpira nje
Dakika ya 39 Shikalo anaanzisha mashambulizi kwa Yanga, All anaokoa ndani ya 18
Dakika ya 38 Waarabu wanacheza faulo kwa All All Dakika ya 37 Makame anaokoa shambulizi ndani ya 18Dakika ya 35 Shikalo anaanisha mashambulizi kwenda kwa waarabu
Dakika ya 34 Juma Abdul anatafuta njia kwenda kwa waarabu
Dakika ya 33 Pyramids wanaanzisha mashambuliziDakika ya 32 Waarabu wanafanya shambulizi kwa Yanga
Dakika ya31 Shikalo anaanzisha mashambulizi kwenda kwa waarabu

Dakika ya 30 Sonso kwa Ally Ally wanapoteza umiliki Yanga.

Dakika ya 29 Papy Tshishimbi anaonyeshwa kadi ya njanoDakika ya 28 Waarabu wanapaisha kwa Shikalo
Dakika ya 27 Mrisho Ngassa anaonyeshwa kadi ya njano kwa kucheza rafu
Dakika ya 26 Sidney anacheza rafu akiwa ndani ya 18
Dakika ya 25 Yanga wanarusha kwenda kwa waarabu
Dakika ya 24 Ally Ally anapeleka mashambulizi kwa Waarabu

Dakika ya 23 Sonso anapiga mpira wa adhabu hauzai matunda
Dakika ya 22 Juma Abdul anapiga faulo inapigwa kichwa na Ally Ally inapaa anaganiDakika ya 21 Ngassa anapiga faulo haileti matunda
Dakika ya 20 Juma Abdul anachezewa rafu na waarabu

Dakika ya 19 Free kikck ya waarabu haizai matunda

Dakika ya 18 nahodha wa Pyramids anachezewa rafu na Ally Dakika ya 17 Mlinda mlango wa Mwarabu anataka kufanyiwa huduma ya kwanza
Dakika ya 16 Fei anacheza faulo kwa mwarabu
Dakika ya 15 Fei Toto anampa Makame safari kwa waarabu
Dakika ya 14 mchezaji wa mawarabu anacheza faulo kwa kugusa mpira.
Dakika ya 13 Yondani anaanzisha mashambulizi kwenda kwa waarabu
Dakika ya 12 Waarabu wanaanzisha mashambulizi
Dakika ya 11 Shikalo anaokoa shuti lililopigwa nawaarabu ndani ya 18.

Dakika ya 10 Kelvin Yondan amekoa hatari iliyokuwa inazama ndani ya nyavu jumla

MCHEZO wa kimataifa kati ya Yanga na Pyramids unaendelea uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mashabiki wamejitokeza kuipa sapoti Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa kimataifa kwa Tanzania.

Mpaka sasa hakuna timu iliyoona lango la mpinzani ikiwa ni kipindi cha kwanza.

Comments are closed.