The House of Favourite Newspapers

Unahitaji Milioni 10 Fasta? Tazama Video Hii!

BENJAMINI Fernandez mtanzania mjasiriamali amekuja na mbinu mbadala ambayo ni tiba kwa tatizo sugu la ajira linalowakabili watanzania. Fernandez ni mmiliki wa Application ya kufanya miamala yote bila kutumia intaneti nchini inayoitwa NALA.

 

Mjasiriamali huyo alipiga chini mshahara wa shilingi milioni 400 nchini Marekani na kuamua kujiajiri mwenyewe kwa sasa amekuja na shindano lililopewa jina la MAMA KASEMA ambalo litakuwa linakusanya mawazo ya kibiashara kutoka kwa watu mbalimbali.

 

Atakayekuwa na wazo bora zaidi ya wengine wote atakuwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10 za Kitanzania.

 

Akizungumza wakati wa kutambulisha shindano hilo, jana katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Makampuni ya Global Group, Fernandez alisema kuwa shindano hilo lipo kwa ajili ya kufikia watu ambao wamekuwa na uhitaji wa msaada wa mitaji ya kuanzisha au kuendeleza biashara zao.

 

“Mimi kama Mtanzania, nasikia furaha na fahari kufanya kitu nchini kwangu ambacho kitakwenda kuwasaidia na watu wengine kama mimi nilivyosaidiwa baada ya kufeli huko Marekani na nikaweza kufikia malengo yangu,” alisema Fernandez.

Comments are closed.