The House of Favourite Newspapers

AVEVA LIVE: Sakata la Pointi 3 za Kagera, Simba Kuishtaki TFF kwa FIFA

0

LEO May 3, 2017 katika Makao Makuu ya Klabu ya Simba, Kariakoo jijini Dar es Salaam, Rais wa timu hiyo Evans Aveva ameongea na waandishi wa habari kuhusu kamati ya haki na hadhi za wachezaji kuipokonya Simba point 3 ilizokuwa imepewa na bodi ya Ligi kutoka kwa Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi aliyekuwa anadaiwa kuwa na kadi 3 za njano.

Kuhusiana na maamuzi hayoa yaliyotolewa na TFF kupitia kwa katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa na kusema Simba haiwezi kukata rufaa tena, Rais wa Simba Evans Aveva ametangaza msimamo wao ikiwemo kwenda FIFA na kulipeleka suala hilo katika mahakama ya kimichezo CAS.

Evans Aveva akizungumza na wanahabari

PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply