The House of Favourite Newspapers

Eric Shigongo: Tengeneza Sifa Njema, Utayapata Mafanikio

MWALIMU na Mhamasishaji maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric James Shigongo amewaasa vijana kutengeneza sifa njema katika jamii ikiwa ni moja ya kutengeneza njia bora za kufanikiwa katika maisha.

Shigongo ameyasema hayo leo wakati akifundisha mbinu za kufanikiwa katika kipindi cha kinachorushwa LIVE kupitia Global TV Online kila Ijumaa saa 10:00 jioni kikiwa na lengo la kuwahamasisha vijana na kuwapa mbinu mbalimbali za kufanikiwa katika maisha yao.

“Leo nitakuwa nafundisha namna ya kujenga REPUTATION kwenye session yetu ya wiki hii ya , lazima ujiulize, unaishi ulimwenguni lakini unatengeneza sifa gani…? Sifa ya MTU hutengenezwa “.

” REPUTATION inajengwa na wewe mwenyewe au mazingira yanayokuzunguka, REPUTATION inaweza ikaharibiwa na mazingira ama wewe mwenyewe, kutokana na tabia unazozijenga.”

” Kila unapoishi jitengenezee tabia ya kutengeneza SIFA njema, kila unachokifanya unatengeneza ‘sifa’ ya aina fulani kwenye maisha yako, katika ulimwengu huu tukubali tukatae unaweza kuharibu sifa/reputation yako kwenye jamii yako “

“Kubadilika in maamuzi.. Its a choice, ukiendelea hivyo sifa hiyo mbaya itaendelea kwa vizazi vyako vijavyo, kuna hatua kadhaa za kupitia kama unataka kubadilisha sifa yako kwenye jamii..”

“Hatua ya kwanza; Jaribu kuwa bora zaidi kuliko ulivyokuwa Jana. Hakuna mtu asiyefanya makosa, we can change our stories, you can change your story… Fanya maamuzi sahihi ya kubadilika “

“What are you choosing toda Nataka leo ufanye maamuzi ni wapi unapotaka kuwa Kwenye sifa mbaya aka nzuri, pigana kadri unavyoweza kutetea na kulinda sifa/reputation, heshima na image yako…”

” Hakuna MTU anayependa kujihusisha na watu wenye sifa/ Reputation mbaya, hivyo ni wajibu wetu kubadilika, nakusihi popote ulipo kuchukua hatua ya kubadilisha maisha yako. Inawezekana ukichukua hatua.”

“Unayo thamani Kwenye ulimwengu huu,Mungu alikuumba akijua wewe ni nani, tembea kifua mbele ukiamini you are POWERFUL”

“Its not easy, kuwa GREAT ni vita, ni mapambano, ni kujinyima, ni kuumia. GREATNESS hides itself behind death. Be the BEST in whatever it is that you are doing. Hata wakiongea unaweza kuwa THE BEST… So be THE BEST! ” – alisema

TAZAMA VIDEO: ERIC SHIGONGO AKIFUNDISHA

Comments are closed.