The House of Favourite Newspapers

SIMBA YAIPIGA SINGIDA BAO 4- 0 UWANJA WA TAIFA

Kikosi cha timu ya Singida Kilichoanza dhidi ya Simba leo Uwanja wa Taifa.
MPIRA UMEKWISHAA DAKIKA 93
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Kwasi anachonga kona fupi kwa Kichuya lakini mpra unaishia miguuni mwa mabeki wa Singida
Dk  88, Kichuya nusura afunge bao la tano baada ya Manyika na beki wake kujichanganya. Kona….
Dk 84 Kotei yuko chini baada ya kugongwa na Mudathiri
Dk 82, Batambuzi anajaribu kuingia katika eneo la hatari lakini Kotei anaondosha
Kikosi cha timu ya Simba kilichoanda dhidi ya Singida leo.

SUB Dk 79 Anatoka Kutinyu na nafasi yake inachukuliwa na Kagoma upande wa Singida
GOOOOOOOOO Dk 75, pasi nzuri ya Kichuya, Okwi anaingia na kuachia mkwaju wa chinichini na kuandika bao la tatu kwa Simba
DK 74, Shiza Kichuya peke yake akiwa amebaki na goli, baada ya pasi nzuri ya Okwi anatoa mpira njeeeee

GOOOOOOOOO Dk 75, pasi nzuri ya Kichuya, Okwi anaingia na kuachia mkwaju wa chinichini na kuandika bao la tatu kwa Simba
DK 74, Shiza Kichuya peke yake akiwa amebaki na goli, baada ya pasi nzuri ya Okwi anatoa mpira njeeeee
Dk 71 Batambuzi anajaribu vizuri kabisa hapa kutoka mbali Manula anauona
Dk 69, Okwi anajaribu kuingia lakini Singida wako makini hapa

Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya Kichuya kushinda bao la kwanza kipindi cha kwanza.

SUB Dk 65 Emmanuel Okwi anaingia kuchukua nafasi ya Muzamiru Yassin
Dk 64 Mundia akiwa katika nagasi nzuri anapaisha juuuuu
Dk 64, Manyika anatoka vizuri na kumuwahi Kichuya vizuri kabisa

Dk 51, Manula anafanya kazi ya ziada, anatoka na kuokoa vizuri dhidi ya Lubinda. Yuko chini akitibiwa
Dk 50, krosi ya Kutinyu, Kambale anachupa na kupiga kichwa safi kabisa, goal kick
Dk 48, pasi nzuri tena ya Ndemla, Kichuya anauwahi na kuachia mkwaju mkuuuubwaaa

Dk  45, mpira umeanza na Simba wamefika katika eneo Kichuya anachia mkwaju mdhaifu

Asante Kwasi akishangilia na wachezaji wenzie baada ya kutupia bao la pili.

MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA

Dk 41, Kaseke anajaribu kuachia mkwaju mkali hapa, Manula anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 35 Kichuya anaingia vizuri, anawekwa chini hapa, mwamuzi anasema twende mbele
Dk 33, Singida wanapata kona baada ya Kotei kuutoa nje mpira. Inachongwa wanaokoa na kwua goal kick
Dk 26, Simba wanagongeana vizuri tena, Ndemla anaingia vizuri lakini Manyika anatokea kwa ustadi mkubwa na kudaka

GOOOOOO Dk 25, Ndemla anatoa pasi safi kwa Kwasi, anaweka kifuani na kuandika bao la pili kwa Smba

Dk 23, Bocco anaingia vizuri, anaachia mkwaju lakini Manyika anaokoa na kuwa kona
SUB Dk 22, Kazimoto anatoka nafasi yake anaingia Said NdemlaDk 20, Singida wanaendelea kusukuma mashambulizi lakini Simba wako makini
Dk 17, Gyan anaingia vizuri na kuachia mkwaju, unatoka sentimeta chache kwenye lango la Singida
Dk16 Singida wanagongeana vizuri na Kutinyu anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, Asante Kwasi anaokoa
Dk 13, Simba inapata kona ya kwnaza baada ya kumtoka beki Singida aliyewahi na kuutoa. Inachongwa lakini haina kitu
Dk 12, Gyan yuko chini baada ya kupigwa teke na Makasi
wakati akijaribu kuuwahi mpira
Dk 13, Simba inapata kona ya kwnaza baada ya kumtoka beki Singida aliyewahi na kuutoa. Inachongwa lakini haina kitu
Dk 12, Gyan yuko chini baada ya kupigwa teke na Makasi
wakati akijaribu kuuwahi mpiraDk 10, Bocco anautokea mpira vizuri mabeki Singida wakidhani ameotea
Dk 8 sasa, Simba wanaonekana kupadhibiti katikati ya uwanja zaidi na kuwapa wakati mgumu viungo wa Singida akiwemo Kutinyu
Dk 5 Simba wanashambulia tena, Manyika anatoka anachelewa Batambuzi anawahi na kuokoa
GOOOOOOOO Dk 3 Kichuya anaruka na kupiga tik tak mbele ya Rushenshagoga na kuandika bao la kwanza kwa Simba
Dk 3, Simba wanapata nje karibu na n alango la Singida
Dk 1, mechi imeanza kwa kasi na Singida wanakuwa wa kwanza kufika katika goli la Simba na mpira uliopigwa na Kambale unakuwa goal kick

PICHA: MUSA MATEJA NA RICHARD BUKOS |  GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.