The House of Favourite Newspapers

LIVERPOOL MAJARIBUNI LEO TENA, KUKIPIGA NA CHELSEA

LIVERPOOL wapo kwenye mtihani mkubwa leo wakati watakapovaana na Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Huu ni mchezo ambao tayari umeshakuwa gumzo hapa England kuanzia nilipowasili hapa mwanzoni mwa wiki hii ambapo mashabiki wamekuwa wakihofi a kuwa Chelsea wanaweza kuzuia mbio za ubingwa za majogoo wa Anfi eld.

 

Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Porto Jumanne iliyopita, mashabiki hawakuwa na mashaka sana na mchezo ule bali gumzo kuu lilikuwa mchezo huu wa leo.

 

Liverpool kwa sasa ndiyo wapo kileleni kwenye Ligi Kuu England wakiwa na pointi 82, wakiwa mbele kwa Man City wenye pointi 80 lakini wenyewe wamecheza mchezo mmoja pungufu ya Liver.

Liverpool itakuwa kwenye Dimba la Anfi eld ambapo itatakiwa kupata ushindi tu ili kuendelea kujihakikishia nafasi ya kukaa kileleni na kuendelea kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kupita miaka 29.

 

Mohamed Salah, amekuwa mchezaji muhimu sana kwenye timu hiyo msimu huu na ndiye anategemewa kuwa anaweza kufanya mambo makubwa kwenye mchezo huu.

 

Hata hivyo, Chelsea ambao nao wanatafuta nafasi ya nne bora kwenye Ligi Kuu England wanataka kupata ushindi kwenye mchezo huu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

 

Chelsea kwa sasa wapo katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 66, lakini endapo wakipoteza wanaweza kushushwa na Arsenal ambao wapo nafasi ya tano na pointi 63. Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri, juzi alisema kuwa anaamini timu yake inaweza kufanya vizuri kwenye mchezo huu kwa kuwa wanataka kufanya vizuri kwenye ligi.

NA SALEH ALLY, LIVERPOOL

Comments are closed.