The House of Favourite Newspapers

Lockerbie, Raia wa Libya Afikishwa Mahakamani Marekani Akitumiwa Kuangusha Ndege

0
Abu Agila Mohammad Masud Kheir Al-Marimi.

Afisa wa ujasusi wa Libya anayeshutumiwa kutengeneza bomu lililotumika kuiangusha ndege ya Pan Am na kuua watu 259, waliokuwa ndani ya ndege na 11 wakiwa chini, huko Lockerbie, Scotland, amefikishwa mahakamani mjini Washington, Marekani.

Abu Agila Mohammad Masud Kheir Al-Marimi, anashutumiwa kwa uhalifu huo wa mwaka 1988 ambao umetajwa kuwa tukio la kigaidi la kimataifa.

Wizara ya sheria ya Marekani ilitangaza Jumapili kwamba Masud alikuwa amekamatwa, miaka miwili baada ya kufunguliwa mashtaka yanayohusiana na shambulizi hilo.

Maafisa wengine wa ujasusi wa Libya wamefunguliwa mashtaka nchini Marekani kwa kushiriki katika tukio hilo lakini Masud amekuwa wa kwanza kufikishwa katika mahakama ya Marekani kuhusiana na kesi hiyo.

Ndege iliyokuwa inaelekea New York, ililipuka chini ya saa moja baada ya kupaa kutoka London, Desemba 21, 1988. Ilikuwa imebeba raia kutoka nchi 21, waliofariki. Miongoni mwao walikuwa Wamarekani 190.

AHMED ALLY AFICHUA SIRI ya USAJILI wa MANZOKI, NTIBAZONKIZA na ADEBAYOR…

Leave A Reply