The House of Favourite Newspapers

Lowassa Amjulia hali Balozi wa zamani Dr. Ahmed kiwanuka

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa akiongea jambo na Balozi wa zamani Dr. Ahmed M kiwanuka (kulia).

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa leo amefika kumjulia hali mwanadiplomasia mkongwe na Balozi wa zamani Dr. Ahmed M kiwanuka anaesumbuliwa na maradhi nyumbani kwake eneo la Upanga, Dar es salaam.

 

Balozi Dr. Kiwanuka amewahi kuwa Balozi katika nchi mbali mbali kama vile India na Indonesia pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Kagera na Rukwa.

 

Awali aliwahi kuwa msaidizi wa Mh. Lowassa. Akizungumza baada ya mazungumzo hayo Balozi Dr. Kiwanuka
amempongeza Mh. Lowassa kwa kitendo cha kurudi ‘nyumbani’.

“Nampongeza sana Mh. Lowassa kwa maamuzi yake ya busara ya kurejea kwenye chama chake cha CCM. Nimefurahishwa sana.
Mwenyezi Mungu amuongoze katika yote.” Aliongeza Dr. Kiwanuka.

 

Akizungumzia mwenendo wa serikali ya awamu ya tano, Dr. Kiwanuka amepongeza uwepo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali inayoongozwa na Rais Dr.John P. Magufuli ikiwemo mradi wa Treni ya mwendokasi (SGR), Mradi wa umeme (Stiegler’s gorge), upanuzi wa bandari ya Dar es salaam na mingine mingi. Pia alimpongeza Rais Dr. John Magufuli kwa kurudisha nidhamu ya watumishi wa umma kitu ambacho kimeboresha huduma kwa wananchi kwa kiasi kikubwa.

Comments are closed.