The House of Favourite Newspapers

Lowassa na Rostam Aziz Ndani ya CCM – Pichaz 10

WAZIRI Mkuu wa zamani na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa jana Ijumaa Machi 1, 2019 alitangaza uamuzi wa kuondoka ndani ya chama hicho alichodumu kwa zaidi ya miaka mitatu na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

Lowassa amerejea katika chama chake cha zamani shughuli iliyofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Katika zoezi la kurejea CCM, Lowassa aliambatana na swahiba wake wa muda mrefu ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Igunga na mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz.

Tazama picha hapo chini.

 

LOWASSA BAADA YA KUREJEA CCM

Comments are closed.