The House of Favourite Newspapers

Mwili wa Joseph Senga Waagwa Dar

0

Kuagwa Senga (3)

Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa akiaga mwili wa Joseph Senga.

Kuagwa Senga (4)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Kuagwa Senga (6)

Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe naye akitoa heshima zake.

Kuagwa Senga (7)

Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa akiaga mwili wa marehemu.

Kuagwa Senga (9)

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea naye akimuaga Senga.

Kuagwa Senga (10)

Mbunge wa Jimbo la Kibamba John Mnyika akitoa heshima zake kwa marehemu Senga.

Kuagwa Senga (5)

Kuagwa Senga (11)

Kuagwa Senga (8)

Waombolezaji wakizidi kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Senga.

Kuagwa Senga (15)

Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akiaga mwili wa marehemu.

Kuagwa Senga (14)

Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu.

Kuagwa Senga (16)

Mpiga picha Mkuu wa Global Publishers, Richard Bukos akiaga mwili wa Senga.

Kuagwa Senga (12)

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda akimuaga Senga.

Kuagwa Senga (13)

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akiaga mwili wa marehemu Senga.

Kuagwa Senga (1)

Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe akitoa pole kwa familia ya marehemu.

Kuagwa Senga (2)

Kutoka kushoto ni Kubenea, Lowassa na Nape wakimsikiliza Mbowe.

Kuagwa Senga (17)

Nape na Mbowe wakibadilishana mawazo.

Kuagwa Senga (18)

Kutoka kushoto ni Kubenea, Lowassa, Nape na Mbowe wakiwa msibani hapo.

Kuagwa Senga (19)

 Jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga likiwa mbele ya waombolezaji.

WAZIRI Mkuu Mstaafu ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Ngoyai Lowassa leo ameongoza waombolezaji waliojitokeza viwanja vya Tip, Sinza jijini Dar es Saalam kumuaga mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga aliyefariki dunia tarehe 27 Julai 2016, akiwa kwenye matibabu ya moyo nchini India.

Baadhi ya viongozi wengine mashuhuri waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa.

Pia wahariri na waandishi mbalimbali wa habari wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda nao wameshiriki kumuaga mwandishi mwenzao.

Marehemu Joseph Senga anatarajia kuzikwa kesho Kwimba jijini Mwanza huku mazishi yake yakihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo mmiliki wa Gazeti la Tanzania Daima, Freeman Mbowe, ambako marehemu Senga alikuwa akifanya kazi.

Jina la marehemu Senga lilikuwa maarufu sana baada ya kupiga picha tukio la kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa Channel Ten, Daud Mwangosi  huko Nyororo mkoani Iringa Septemba 2, 2012.

Julai 27, 2016 siku ambayo hukumu dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi ilikuwa inatolewa ndiyo siku mauti yalimfika Senga huko nchini India alipokuwa kwa matibabu ya moyo.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Joseph Senga mahali pema peponi. AMEN.

Leave A Reply