The House of Favourite Newspapers

Kangi Lugola Ampa Maagizo Mengine IGP Sirro

WAZIRI Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Pilisi nchini, IGP Simon Sirro, kupunguza vituo vya ukaguzi wa magari visivyo na lazima ambavyo vimeonekana kutumiwa vibaya na askari wa usalama barabarani wasio waadilifu.

 

Lugola ameyasema hayo leo Jumatano, Oktoba 3, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake Mjini Mbeya akitokea mkoani Rukwa na kusema vituo hivyo ambavyo vilivyowekwa baada ya kila hatua 20 kwa lengo la kudhibiti ajali, vimegeuzwa na kuwa fursa kwa baadhi ya askari.

 

“Askari wamekuwa wakiwaumiza wananchi, wanasimamisha magari kila kituo, vituo vipo kila zaidi ya hatua 20, halafu kazi kubwa ni kuomba na kupokea rushwa,” amesema Lugola.

JPM “Mstaafu Mwinyi ninakuhusudu kweli kweli”

Comments are closed.