The House of Favourite Newspapers

Lukuvi Aonya: ‘Msiijaribu Serikali’ – Video

0

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  William Lukuvi, amewaonya wananchi wanaojenga mijini bila kufuata utaratibu.

 

Ametoa onyo hilo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani jijini humo wakati akikagua nyumba ambazo zimejengwa bila kufata utaratibu na kukosa vibali vya ujenzi.

 

Waziri huyo alifikia hatua ya kusimamisha ujenzi kwa kuziwekea alama nyumba ambazo ujenzi wake umekiukwa na kuwaamuru wamiliki kusitisha shughuli zote hadi wafuate utaratibu.

 

Hata hivyo,  amesema serikali haina mpango wa kubomoa nyumba za wananchi isipokuwa wananchi wanatakiwa kujenga kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata vibali vya ujenzi.

 

Leave A Reply