The House of Favourite Newspapers

Lulu Afunguka Kuhusu Kila Mwanaume Anayetembea Naye Anakufa

lulu-1Na Imelda Mtema | Gazeti la Risasi Mchanganyiko

DAR ES SALAAM: Tumempata! Baada ya miaka mingi ya minong’ono juu ya mambo mbalimbali yanayomhusu staa mdogo lakini mwenye jina kubwa katika Bongo Muvi, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, hatimaye Risasi Mchanganyiko limempata na kufanya naye mahojiano ya ‘maana’ ndani ya Ukumbi wa Landmark Hotel, iliyopo Mbezi jijini Dar.

Lulu, ambaye kila wakati anaonekana nadhifu na mwenye mvuto wa kipekee, alifunguka wakati alipokutwa katika sherehe za bethidei ya mtoto wa Muna, aitwaye Patrick iliyosheheni watoto wengi waliofika kumuunga mkono.

Risasi: Kuna madai kuwa unajitenga na mastaa wenzako na unaringa, zikoje habari hizi?

Lulu: Nasikia wanazungumza hivyo, lakini ukweli ni kuwa nimebadilisha kidogo staili ya maisha yangu, ni bora kujitenga kwa ajili ya usalama wangu, lakini kwenye vitu vya muhimu kama misiba na vitu vingine tupo pamoja.

Risasi: Unamaanisha nini kwa ajili ya usalama wako?

lulu-3Elizabeth Michael ‘Lulu’

Lulu: Kwa sababu panakuwa na watu mbalimbali hivyo  kuna vitu vingi  vinavyoweza kuniharibia mimi.

Risasi: Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa una ujauzito, tena mkubwa tu, vipi umeharibika?

Lulu: Kama hizi mimba za kuambiwa zingekuwa kweli, basi ningeshakuwa na watoto hata saba jamani, sina mimba kama unavyoniona (akimuonyesha tumbo mwandishi wetu)

Risasi:  Ina maana hupendi kuzaa? Kuna kipindi uliwahi kusema unahitaji kuzaa mapema!

risasi-jumatano-1

Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Toleo la Desemba 21, 2016

Lulu: Ni kweli na ninatamani hata sasa nizae, lakini nataka mtoto wangu awe kwenye msingi thabiti kabisa, sitaki apitie kama niliyopitia huko nyuma, kulelewa na mzazi mmoja na shida nilizopata, bado najipanga.

Risasi: Yale madai ya kuvishwa pete na ndoa nayo yakoje?

Lulu: Hapana, sijavalishwa pete, wala siko mbioni kuolewa. Ndoa siyo kitu cha kulazimishana, kitu ambacho kinatoka moyoni kwa mtu bila kukilazimisha,  maana ndoa ukiilazimisha baadaye ndiyo yanaibuka matatizo makubwa.

steven-kanumbaMarehemu Kanumba enzi za uhai wake

Risasi: Lulu, kuna haya maneno kuwa kila mwanaume unayetoka naye anafariki, hivi likoje na pengine linakuathiri vipi katika maisha yako?

Lulu: Kwa kweli haliniathiri chochote kwa sababu sioni mantiki. Una maana mimi nimetoka na wanaume wawili tu tangu nizaliwe? Nimetoka na wanaume wengi na wapo wanaendelea na maisha yao kama kawaida, hiyo inatokea tu kama kifo kwa watu wengine.

Risasi: Nakuona uko na watoto wa mpenzi wako (kibosile wa redio) hapa inakuaje hiyo?

lulu-2Lulu: Kwanza hawa watoto wananipenda sana, lakini kingine mdogo wangu amezoeana nao kwa sababu umri ni mmoja na mimi napenda watoto.

Risasi: Vipi kuhusu bifu lako na Hamisa Mabeto?

Lulu: Sina bifu na mtu, lakini pia siwezi kukataa moja kwa moja labda inatokana na mtu anavyozungumza huko nje, kwa kuwa lisemwalo lipo watu hawawezi kukurupuka tu.

Risasi: Ni kipindi kipi  kigumu ulichopitia katika maisha yako?

mobetoHamisa Mobeto

Lulu: Kipindi ambacho nilikuwa gerezani, jamani siwezi kuumia katika maisha yangu kama kipindi kile.

Risasi: Kuna kipindi ambacho ulikuwa ukisoma pale Magogoni, bado unaendelea na shule na ulikuwa ukisomea nini?

Lulu: Ndiyo nimemaliza kama wiki moja iliyopita na pale nilikuwa nisomea mambo ya Rasilimali watu (Human Resource)

Risasi: Kutokana na changamoto ulizopitia unawaambiaje wasichana wenzako?

Lulu: Wasikate tamaa wanapokutana na magumu, wapambane tu.

Risasi: Kuna kipindi ulikuwa unaenda kanisani na kama ulikuwa umeokoka, mpaka sasa unaenda?

Lulu: Nitafanyaje mambo yangu bila kumshirikisha Mungu? Bado naenda kanisani kama kawaida.

Risasi: Nakushukuru Lulu kwa ushirikiano wako.

Lulu: Asante na karibu.

Comments are closed.