The House of Favourite Newspapers

Lulu Atoa Msaada Kwa Wasichana Akiwa Gerezani

MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa sasa anaendelea kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji mwenzake, Steven Kanumba, mnamo April 7, 2014,  ametoa mchango wake wa pedi kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike katika kampeni ya ‘Namthamini’ inayoendeshwa na uongozi wa kituo cha televisheni cha EATV cha jijini Dar es Salaam.

 

Zawadi hizo  ziliwakilishwa na msanii mwenzake, Mahsein Awadh Said maarufu kwa jina la Dr Cheni jana katika ofisi za EATV Mikocheni jijini Dar es Salaam aliposema anaamini kampeni hiyo italeta mabadiliko makubwa kwenye jamii ya sasa kutokana na matatizo wanayokumbana na watoto wa kike walioko mashuleni.

 

Alichokiandika Dr Cheni kupitia akaunti yake ya Instagram:-

Hongera sana @elizabethmichaelofficial (LULU) Kwanza niwapongeze kwa hii program nimekuwa mfuaatiliaji na naamini itakuwa na ‘Impact’ kubwa kwenye jamii. Kikubwa mimi Mahsein @drchenitz ni Muwakilishi, nimeleta ‘pic kadhaa za Pads ambazo zitakuwa msaada kwa Wasichana wakitanzania  Huu ni mzigo wa Elizabeth Michael (LULU),  Ameomba niwasilishe kwenu. Nimekuwa nikimtembelea mara kadhaa kumjulia hali na yeye ameomba ashiriki kwenye kampeni hii ingawaje hayupo. Yupo (jela) Zaidi amesema niwaambie. ANAWAPENDA saana, na anawataka mabint wa kitanzania wawe huru katika kutimiza malengo yao, wasikate tamaa na Mungu atawasimamia.

Comments are closed.