The House of Favourite Newspapers

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAAHIDI KUMTETEA MAGUFULI

Naibu katibu Mkuu CCM Bara, Rodrick Mpogoro,(katikati) akimkabidhi cheti mmoja wa wanajumuiya hiyo kutokana na mchango wake katika chama.
...Mpogoro (kulia) akimkabidhi mbunge wa zamani wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan kutokana na mchango wake katika jumuiya hiyo.
Mpogoro akiwapongeza wajumbe wa jumuiya hiyo.
Naibu katibu Mkuu CCM Bara, Rodrick Mpogoro akihutubia.
Mkutano wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam ukiendelea.

 

Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, imeahidi kuendelea kumtetea Rais Magufuli dhidi ya watu wanaombeza na kudharau kazi kubwa ya kuiletea maendeleo nchi anayoifanya.

 

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rodrick Mpogoro, katika Mkutano wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere, Posta jijini Dar es Salaam.

 

Katika hotuba yake, Mpogoro amewataka wanajumuiya hiyo kuwa wamoja na imara katika kutekeleza azma ya chama hicho  kuendelea kukua katika mashina mbalimbali ya serikali za mitaa.

 

Comments are closed.