The House of Favourite Newspapers

LULU DIVA AAHIDI NDOA, MTOTO 2019

Lulu Abbas ‘Lulu Diva

MWANAMUZIKI na mwigizaji wa filamu Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ameweka ‘pleini’ kuwa lazima mwaka unaokuja na yeye ajikwamue kwa kujitoa kimasomaso kuolewa au hata kupata mtoto, hicho ndicho kikubwa alichokipanga kichwani mwake.  

 

Lulu Diva aliliambia Ijumaa kuwa, kwa kazi yake ya muziki anayoifanya hivi sasa, anahitaji kufanya kitu ambacho huko mbeleni hakitampa kikwazo kama kupata mtoto mapema ili akiwa anaendelea kumtafutia maisha, yeye anaendelea kukua.

 

“Ni vizuri sana kujipangia malengo ya kimaisha na mimi ndiyo hivyo nimeshapanga ninachokitaka mwakani kwa sababu maisha yenyewe ni mafupi. 2019 nikifanikiwa kupata ndoa ni heri, lakini hata kama nitapata mtoto nitashukuru pia,” alisema Lulu Diva.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.