The House of Favourite Newspapers

LULU DIVA ADAIWA KATUPIWA JINNI

JAMANI wapenda ubuyu mtamu mpo? Basi kwa taarifa yenu ubuyu wa motomoto Pasaka hii unamhusu mwanamuziki wa kike anayefanya poa kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

Kwa mujibu wa mtoa ubuyu wetu ambaye ni mtu wa karibu wa Lulu Diva, mwanadada huyo anadaiwa kutupiwa jini na mke wa mtu baada ya kumchukulia mumewe miaka kadhaa iliyopita.

Inasemekana kwamba, jini huyo kazi yake ni kumharibia Lulu Diva ili asipate mwanaume wa kumuoa badala yake awe anahangaika na wanaume tu hadi uzeeni kwake.

“Ninyi muulizeni kama baada ya tukio hilo la kutupiwa jini, kuna mwanaume yeyote ambaye amewahi kutulia naye?

MAHARI YARUDISHWA

“Kila mwanaume aliyempata aliingia mitini. Kama ni kuolewa, basi Lulu Diva angeolewa mwaka jana mwishoni, lakini mchumba huyo alipobaini anatoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake, akaomba mahari yake irudishwe maana alikuwa ameshatoa kabisa mahari,” kilisema chanzo.

HUYU HAPA LULU DIVA

Baada ya kuumung’unya ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Lulu Diva na kumuuliza juu ya jambo hiyo ambapo mambo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Lulu Diva?

Lulu Diva: Poa tu, naona leo kuna ishu.

Ijumaa Wikienda: Ni kweli kuna ishu kwelikweli maana hapa kuna ubuyu kuwa uliwahi kutupiwa jini na mke wa mtu ndiyo maana huwa hutulii na mpenzi mmoja au huolewi. Je, hii ishu ikoje?

Lulu Diva: Kwanza niseme, huyo aliyewaambia nimeshamjua maana ni mimi mwenyewe niliamua kumwambia ishu hiyo.

Isitoshe mimi nilitoa siri hiyo kwa sababu kila mipango yangu ya ndoa ikikamilika, kunatokea jambo na mwanaume anasema ana mambo yake mengine.

Hapo kama siyo kupigwa juju ni nini? Hilo la kwamba aliyenipiga juju ni mume wa mtu ni siri yangu.

Ijumaa Wikienda: Je, utaishi hivyo hadi lini?

Lulu Diva: Ninamuomba Mungu aniondolee huyo jini ili siku moja na mimi nimpate wangu wa kufa na kuzikana, tudumu hadi kifo kitutenganishe.

Comments are closed.