The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva Akiri Kuporwa Gari

0

Sexy lady wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amekiri kuporwa lile gari la bei mbaya aina ya Jeep.

IJUMAA WIKIENDA linafahamu kwamba, Lulu Diva alipewa gari hilo la kifahari na mwanaume aliyejulikana kwa jina la Joh ambaye alikuwa mpenzi wake kabla ya kutofautiana mwishoni mwa mwaka jana.

 

Lulu Diva alifafanua ishu hiyo ya kuporwa alipokuwa akizindua duka lake kubwa la vyakula na mboga liitwalo Divana Sokoni lililopo maeneo ya Mbezi-Beach, Dar.

 

“Ni kweli lile gari nimepokonywa, limechukuliwa na mwenye gari lake.“Kama kuna wanaosema nimeliuza lile gari si kweli bali nimepokonywa na mwenyewe, watu waelewe maisha yamebadilika na mimi sina gari kwa hiyo watu wakikutana na lile Jeep wajue siyo la kwangu tena,” anasema Lulu Diva.

 

 

“Limetokea lililotokea kwa sababu sikuzaliwa na gari, mimi nafanya kazi hivyo najua ipo siku nitanunua gari lingine,” alisisitiza. Lulu Diva alizawadiwa gari hilo mwaka 2017 likiwa na thamani ya shilingi milioni 300 za Kitanzania.

Stori; iMelda MteMa, Dar

Leave A Reply