Lulu Diva: ‘Mgonjwa’ Wa Kioo (Mpaka Home)

      lulu-diva-10 Muuza sura kwenye video za Kibongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ akiwa nyumbani kwake Mitaa ya Kinondoni Vijana jijini Dar.

Na Imelda Mtema

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa Mpaka Home? Spidi ni ileile 120 ya kukupa fursa ya kuweza kuwafahamu vyema mastaa mbalimbali pamoja na maisha yao halisi wakiwa nyumbani.

lulu-diva-5

Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ akiwa anasoma email zake.

Bila kupoteza ‘time’, namtambulisha kwako staa ambaye leo nimekuletea kwenye safu hii, si mwingine ni muuza sura kwenye video za Kibongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambaye anaishi Mitaa ya Kinondoni Vijana jijini Dar, twende pamoja kujua mengi kuhusu yeye.

Mpaka Home: Mambo vipi Lulu, kwa nini umeamua kuishi mitaa hii, nilikuwa nakutegemea ungekuwa Masaki, Oysterbay na mingine inayoaminika kuwa ya kishua?

 

lulu-diva-11

Lulu akiwaza jambo.

 Lulu: Aah, ni mtazamo tu lakini hata hapa ninapoishi ni mitaa ya kishua na ndio chaguo langu.

Mpaka Home: Kwa uelewa wako, unafikiri nyumba ya staa inatakiwa iweje?

Lulu: Inategemeana na uwezo wa staa mwenyewe, lakini muonekano ni kitu cha muhimu maana hata kama huna pesa kiivyo unaweza kutengeneza ndani kukawa pazuri.

Mpaka Home: Maisha yako ya kawaida yakoje hapa mtaani?

Lulu: Naishi kawaida kama watu wengine tu, yaani ninachotamani kufanya, nafanya. Nikitaka kula muhogo kibandani nafanya hivyo sitaki maisha ya kuigiza.

lulu-diva-7

Akicheza na mbwa wake.

Mpaka Home: Nilipofika hapa nimeshangaa sana kukuta jikoni, kabla nilifikiri mambo ya moto na wewe ni vitu mbalimbali?

Lulu: Nashukuru kwa kuwa umenikuta mwenyewe maana usingeweza kukubali kama napika, lakini mimi chakula mara nyingi tu maana napenda, pia mimi ni mwanamke na upishi ni moja ya majukumu yetu.

lulu-diva-3

Akiwa amepozi.

Mpaka Home: Vipi, hapa unaishi na shemeji nini maana mandhari take si mchezo?

Lulu: Haaaha…haa (anacheka kwa kujiachia), naishi peke yangu bana mimi sijaolewa, lakini kwa sasa yupo mama yangu hapa maana ni mgonjwa.

 Mpaka Home: Nini hasa unachokipenda kwenye nyumba yako?

lulu-diva-8

Akimuwekea mbwa chakula.

Lulu: Napenda usafi. Uchafu ni adui yangu na ndiyo maana unaona ndani kuko hivi.

Mpaka Home: Ukipata wageni ni kitu gani unapenda kuwaandalia ili kuwafurahisha?

Lulu: Kwa upande wa chakula, pilau huwa chaguo langu la kwanza. Nafikiri watu wengi wanapenda, kuhusu kinywaji huwa nawauliza wageni wanapendelea nini!

Mpaka Home: Kila mtu ana sehemu yake ambayo anaipenda nyumbani, kwako wewe ni wapi unapopapenda zaidi?

lulu-diva-6

Lulu akiweka mambo sawa jikoni.

Lulu: Napenda sana kwenye kioo kila mara nikae nijiangalia basi.

Mpaka Home: Hujawahi kufikiria kuwa na nyumba yako?

Lulu: Hicho ndicho kitu kinachoniumiza kichwa kila kukicha. Mambo ya kupanga nimeyachoka kwa kweli, unajua unapokuwa kwako unakuwa na uhuru wa kufanya kila unachotaka kuhusu ndani na mazingira yanayokuzunguka kwa kujiachia na hakuna anayeweza kukuuliza lolote lile.


Loading...

Toa comment