The House of Favourite Newspapers

Serengeti VS Congo-Brazzaville Kupambana Kesho Taifa

kocha-shimeKocha wa Serengeti Boys Bakari Shime(kulia) akiwa na Kocha wa Congo-Brazzaville Ekarik Basile walipokutana mapema leo kuzungumzia mchezo wa kesho.

DAR ES SALAAM, kesho Jumapili kikosi cha timu ya taifa ya vijana, Serengeti Boys kikitarajia kushuka dimbani kumenyana na Congo Brazaville, kocha mkuu wa timu hiyo, Bakari Shime amewataka mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu hiyo kwani ameiandaa vyema kuweza kuibuka na ushindi.

Huu ni mchezo wa mwisho wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za vijana za Mataifa Afrika (Afcon) ambazo zitafanyika mwakani nchini Madagascar ambapo mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa Taifa, Dar.

Shime amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi hapo kesho kushuhudia mtanange huo wa kukata na shoka utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

 “Tuko vizuri na tunawaambia mashabiki waje kwa wingi kuona jinsi tutakavyowapiga hawa Congo Brazzavile, lakini pia wakumbuke wao ndiyo mchezaji wa 12 hivyo uwepo wao pia niu muhimu.” Amesisitiza Kocha huyo.

STORI: SAID ALLY/CHAMPIONI.

Comments are closed.