The House of Favourite Newspapers

LUNGI , KALALA WANASWA KIMAHABA

Kalala Junior.

MSANIi wa filamu za maigizo nchini, Lungi Mwaulanga hivi karibuni alifanya kituko cha aina yake baada ya kunaswa akijibebisha laivu kimahaba ukumbini kwa mwanamuziki wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Kalala Junior. Tukio hilo lilijiri ndani ya Ukumbi wa The Jonz uliopo Magomeni Mwembe-Chai, jjini Dar ambapo bendi hiyo ilikuwa ikitambulisha nyimbo zake mbili, Kibamia ambao ni utunzi wake Msafiri Diouf na Povu uliotungwa na Haji Ramadhani.

Baada ya utambulisho wa nyimbo hizo zilioonekana kumkuna Lungi ambaye alikuwa akionekana ameshapata kilaji cha kutosha ambapo alikuwa akivamia jukwaani kila mara na kuwamwagia wanamuziki noti nyekundu za Msimbazi. Vituko vya msanii huyo havikuishia hapo kwani, Kalala aliposhuka jukwaani alimuita na kuanza kujibebisha laivu mbele ya mashabiki kwa kumkumbatia kimahaba lakini Kalala alionekana kuona aibu kufanya hayo hadharani.

Tukio hilo lilisababisha baadhi ya mashabiki waliofurika ukumbini hapo kuanza kumjadili msanii huyo ambaye alikuwa akimtomasatomasa Kalala hadharani.Wakati Lungi akiendelea kufanya hayo baada ya Kalala kubaini kuwa anafotolewa na paparazi wetu alianza kujinasua kwa msanii huyo huku akimtafadhalisha paparazi wetu asiwafanyie hivyo.

“Aaah! Kaka naomba usitufanyie hivyo, isije ikawa soo nyumbani, si unajua mimi nina waifu, huyu ni shabiki tu ambaye hapa aliniita aniambie kitu nami nilikuja kumsikiliza kumbe mwenzangu keshachangamka,” alisema Kalala.

Paparazi wetu alizungumza na Lungi kuhusiana na tukio hilo ambapo msanii huyo alijibu: “Wee paparazi hebu tuache kama tulivyo, acha kufuatilia mambo ya watu, sisi hapa tumekuja kufurahi, ukitaka kutuhoji tuite studio siyo hapa sehemu ya starehe,” alimaliza kusema Lungi.

STORI: Richard Bukos, Risasi

Comments are closed.