The House of Favourite Newspapers

Lungi: Likiibuka gonjwa litaua mastaa kibao

0

LUNGI (1)STORI: Hamida Hassan, Wikienda

Dar es Salaam: Msanii wa sinema za Kibongo wa kitambo, Lungi Maulanga amefunguka kuwa endapo litaibuka gonjwa la kuambukiza, mastaa kibao wa Kibongo watauana kwani kila kukicha wanachukuliana mabwana, jambo ambalo linahatarisha afya zao.

Akizungumza na Wikienda, Lungi alisema anakerwa na tabia ya mastaa wa kike kuchukuliana wanaume kwani tabia hiyo itawakosti kwa sababu magonjwa mengi ya kuambukiza hutokana na kujamiiana hivyo likiibuka gonjwa kwa mmoja, litasambaa kwa wengi.

“Unakuta staa anakuwa na mwanaume asubuhi, mwenzake anamchukua jioni bila kujali hili ni tatizo kubwa kwani ni rahisi sana kuambukizana magonjwa. Mbaya zaidi mastaa hao wanadiriki kushindana kwa kuwazalia wanaume hao hivyo ni janga la baadaye wao hawalioni,” alisema Lungi.

Leave A Reply