The House of Favourite Newspapers

Lusajo: Nitampoteza Mayele

0

KINARA wa wafungaji kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa, Reliants Lusajo, amemtangazia vita mpinzani wake mkubwa katika vita ya ufungaji bora msimu huu, Fiston Mayele akisema amejipanga kuendelea kutupia mabao kwa kila nafasi atakayoipata.

Lusajo ambaye ni nahodha wa Namungo, mpaka sasa amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao tisa akifuatiwa na Mayele wa Yanga mwenye mabao sita.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Lusajo alisema: “Nafurahia kiwango ambacho nimekuwa nacho kwa sasa, kama mchezaji hususani ambaye ninahudumu kwenye unahodha ni jambo muhimu kuhakikisha ninaipambania timu yangu ili iweze kupata matokeo mazuri.

“Kuhusu vita ya ufungaji bora ni kweli hiyo ni sehemu ya malengo ambayo nimejiwekea msimu huu, najua ushindani ni mkubwa kutokana na ubora wa washambuliaji wengine kama vile Fiston Mayele, lakini nimejipanga kutumia kila nafasi ambayo nitaipata kuhakikisha ninafunga mabao mengi zaidi.”

Joel Thomas, Dar es Salaam

Leave A Reply