The House of Favourite Newspapers

Plan Madini Amtosa Harmonize Kisa Beka Flavour

0

DAMU change kunako Bongo Flevani, Ally Omari almaarufu Plan Madini ambaye hivi karibuni alitangaza kufanya ngoma yake ya Wasiwasi na C.E.O wa Konde Gang, Harmonize amebadili uamuzi huo na kuamua kuifanya ngoma hiyo na Beka Flavour.

 

Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Plan Madini anasema amebadili msimamo huo baada ya kukaa na menejimenti yake na kuamua kufanya ngoma hiyo na Beka ambaye wametoka mbali kimaisha ikiwemo kusoma shule moja ya Sekondari ya Kibaoni iliyopo Ifakara mkoani Morogoro.

 

“Nimeona nikimshirikisha mshkaji ambaye tumesoma wote italeta mzuka zaidi kwani hata yeye mwenyewe ataona nimetambua hilo.

 

Katika kuleta ladha zaidi audio na video; vyote nimetengeneza kwa prodyuza wake, Mafiya ambaye mara nyingi hakosei na hivi tunavyoongea tayari imeanza kuruka kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga,” anasema mwamba huyo.

STORI; IJUMAA SHOWBIZ, DAR

Leave A Reply