The House of Favourite Newspapers

Lynn asema hakuna mwanaume wankumuacha

MREMBO anayetamba kwa sasa na wimbo wake mpya wa Pepea, Irene Louis ‘Lyyn’ kwa mara ya kwanza amefunguka mambo mengi usiyoyajua kuhusu maisha yake ikiwemo kutomposti aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenye mitandao ya kijamii katika siku ya kuzaliwa kwake, Oktoba 2, mwaka huu.  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mikito Nusunusu, Lyyn alieleza mambo kibao kuhusiana na sanaa pia, ungana naye hapa chini:

MIKITO: Hongera sana kwa wimbo mpya wa Pepea, umejitahidi, nini siri ya mafanikio yako?

LYYN: Asante sana, siri ya mafanikio yangu kwanza kabisa ni kukubali kukosolewa lakini pia kuamini kwamba unaweza kufanya jambo fulani na kujituma kadiri uwezavyo.

MIKITO: Idea ya Wimbo wa Pepea uliitoa wapi na kwa nini uliamua kumshirikisha Amigo?

LYYN: Nilikuwa nataka nifanye kitu ambacho ni cha tofauti ndiyo maana umeona hata staili niliyotumia kuimba ilikuwa tofauti hivyo nikaona Amigo ndiye anafaa zaidi.

MIKITO: Uliandikiwa na nani na umerekodi wapi?

LYYN: Aliniandikia Kusah na nimerekodi kwa Mensen Selekta.

MIKITO: Ulipata ugumu gani wakati wa kurekodi wimbo huo?

LYYN: Nilipata ugumu wakati wa kurekodi video kwa sababu tulikuwa tunamtaka mtu ambaye anaweza kuimba vile (kuimba kutokana na aina ya muziki) hivyo ikatubidi tumsubiri yeye mpaka afike ndio tuendelee kurekodi, lakini wakati wa kuimba sikupata ugumu wowote kwa sababu tulirekodi siku moja tena usiku.

MIKITO: Umeshawahi kuwaza kufanya kolabo na msanii mwingine mkubwa hapa Bongo?

LYYN: Yah, nimeshawahi kuwaza na tayari kuna ambao baadhi nimeshafanya nao kolabo bado kushuti tu ili nyimbo ziachiwe.

MIKITO: Wasanii gani?

LYYN: (Anacheka) Sasa nikiwataja sasa hivi nitakuwa nimepoteza ladha yote, mashabiki wangu wakae mkao wa kula tu.

MIKITO: Nani ‘anakumeneji’ katika kazi zako?

LYYN: Sina menejimenti, najimeneji mwenyewe kila kitu lakini siku ikifika nitahitaji menejimenti ambayo ni nzuri na inafanya kazi vizuri kwa sababu nahitaji menejimenti ambayo itanifanya niende mbele zaidi.

MIKITO: Baada ya Pepea tutarajie nini tena toka kwako?

LYYN: Mtarajie kitu kingine kizuri zaidi na cha tofauti kabisa.

MIKITO: Irene sijakuona kwenye Tamasha la Fiesta wala Wasafi Festival tatizo nini?

LYYN: Mimi nahisi muda bado tu, muda ukifika mtaniona kote huko.

MIKITO: Unazungumziaje ishu ya Harmonize kuondoka WCB?

LYYN: Siyo vibaya kawaida tu, kwa sababu ninavyohisi ni kwamba mtu akifanya sana kazi kwenye kampuni flani akapata mishahara yake mingi naye atatafuta kitu chake cha kufanya, kwa kuwa kila mtu anatafuta kwa mbinu yake.

MIKITO: Kati ya video queen na muziki kipi ambacho umekipa kipaumbele sana?

LYYN: Muziki ndiyo nimeupa kipaumbele kwa sababu u-video queen nilishaacha muda mrefu sana tangu nilipoanza kujitambulisha kuwa mimi ni mwanamuziki, hivyo naweza kusema kuwa muziki ndio kila kitu kwangu kwa sasa.

MIKITO: Tangu umeanza muziki mpaka sasa ni mafanikio gani umeyapata?

LYYN: Mafanikio yapo mengi tu lakini naweza nikasema yale mafanikio makubwamakubwa bado yapo njiani hivyo siwezi kuwa muongo sasa hivi na kusema nimepata mafanikio haya wakati bado sijayapata.

MIKITO: Mara yako ya kwanza kupanda stejini kupafomu ulijisikiaje?

LYYN: Nilikuwa na hofu sana, halafu nakumbuka ilikuwa Iringa kwa hiyo nikawa nawaza jamani itakuwaje, unajua ile kitu kama ndio mara yako ya kwanza kukifanya lazima upagawe kidogo, lakini nilipofika pale nikapafomu vizuri hadi watu wakaniambia Lyyn umepafomu vizuri mno.

MIKITO: Basata wanakutambua wewe kuwa ni mwanamuziki?

LYYN: Ndio wananitambua kwa sababu nilishaenda kujisajili.

MIKITO: Huwa unajisikiaje unaposemwa vibaya kuhusu Diamond?

LYYN: Huwezi amini mimi siyo tu kusemwa vibaya kwa ajili ya Diamond lakini chochote tu ambacho mtu atanisema vibaya mimi huwa nacheka, huwa siruhusu kabisa moyo wangu uchukie kisa maneno ya watu.

MIKITO: Nini malengo yako hapo baadaye katika muziki wako?

LYYN: Malengo yangu ni kuja kuitambulisha nchi yangu, kuwa mwanamuziki mkubwa na vitu vingi mbeleni huko.

MIKITO: Msanii gani wa kike Bongo huwa anakupa tabu sana na unatamani uje ufanye naye kolabo?

LYYN: Vanessa Mdee, ananitesa sana na ndio mtu ambaye natamani sana nije kufanya naye kolabo.

MIKITO: Umeshawahi kumfuata na kumuambia?

LYYN: Sijawahi ila nitamfuata siku moja, huwa tunakutana tu na kusalimiana kisha tunapiga stori nyingine lakini siku ikifika nitamfuata.

MIKITO: Kuna tetesi kwamba ulihama Goba ulikokuwa unaishi ni kweli?

LYYN: Ndiyo ni kweli sasa hivi naishi Mbezi Beach.

MIKITO: Mbezi Beach, umejenga, umepanga au umenunua nyumba?

LYYN: (Anacheka) We jua tu naishi Mbezi Beach.

MIKITO: Umeongea katika mahojiano na +255 Global Radio kwamba mwaka jana mpenzi wako alikuzawadia gari na mwaka huu amekuzawadia nyumba ambayo ipo Kigamboni, unaweza kutuambia hiyo nyumba ina thamani gani?

LYYN: Ni kweli nimezawadiwa nyumba na mpenzi wangu ipo Kigamboni lakini siwezi kutaja thamani yake kwa sababu mwenyewe kanikataza hata kuionyesha, hivyo akisikia hatapenda, lakini ni nyumba kubwa imeshakamilika na kuna watu ambao huwa wanaenda tu pale kufanya usafi.

MIKITO: Mpenzi wako ni mtu wa aina gani?

LYYN: Ni mfanyabiashara, gentlemen anayejielewa.

Mikito: Kwa nini humuweki hadharani?

LYYN: Simuweki kwa sababu yeye mwenyewe hapendi kuwekwa kwenye mitandao.

MIKITO: Nani alianza kumuacha mwenzake kati ya wewe na Diamond.

LYYN: Ngoja nikwambie kitu, mimi mpaka mwanaume tunaachana ujue mimi ndio nimetaka, hakuna mwanaume ambaye sitaki kuachana naye nikaachana naye.

MIKITO: Kwa hiyo wewe ndiye ulimuacha Diamond?

LYYN: Wewe elewa hivyo hakuna mwanaume aliyewahi kuniacha ila mimi ndio huwa naacha.

MIKITO: Diamond akihitaji kurudiana na wewe utakuwa tayari?

LYYN: Hapana, haiwezi tena kutokea kwa sababu mimi nina mahusiano yangu ambayo yapo imara.

MIKITO: Kuna kipindi ulikuwa na bifu na Tunda Sebastian lakini baadaye tena tukaanza kuwaona pamoja ilikuwaje mkaanza kuwa pamoja?

LYYN: Sisi hatujawahi kuwa na bifu ila ni watu tu ambao walikuwa wanakuza mambo, Tunda ni rafiki yangu na hata kwenye birthday yangu alikuja.

MIKITO: Watu waliongea sana wewe kuwa na bodigadi wengi kwenye birthday yako (hivi karibuni), unaweza ukafafanua zaidi?

LYYN: Mimi ni lazima nilindwe, halafu mimi mzuri kwa hiyo naweza nikaibwa pia ndiyo maana uliona mabodigadi kama wote pale ukumbini.

MIKITO: Kuna picha inasambaa sana mitandaoni, kuna mdada amelala kitandani akiwa kama alivyozaliwa, wanazengo wanasema ni wewe kuna ukweli wowote.

LYYN: Jamani, picha gani tena hiyo, sijaiona lakini naweza kusema huyo siyo mimi kabisa, mimi siwezi kufanya mambo ya ajabu kama hayo najiheshimu. Sijawahi kuwaza wala kufikiria kupiga picha za utupu wala kujirekodi nikiwa mtupu, watakuwa wamenifananisha.

MIKITO: Kwa nini hukumposti Diamond kwenye birthday yake?

LYYN: Sikumposti kwa sababu na yeye hakuniposti siku ya birthday yangu.

MIKITO: Neno la mwisho kwa mashabiki wako.

LYYN: Nawapenda sana, naomba waende Youtube wakaangalie video ya Pepea na watarajie mambo mengine mazuri.

STORI: MEMORISE RICHARD

Comments are closed.