The House of Favourite Newspapers

Mwili Uliozuiliwa Mloganzila Ukidaiwa Tsh 26m, Wakabidhiwa – Video

WASWAHILI husema subira yavuta kheri, hatimaye familia ya marhemu Mwanaidi Nakari (16) ambaye mwili wake ulikuwa umezuiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kampasi ya Mloganzila kuruhusiwa kuuchukua.

 

Awali haikua rahisi kwa familia ya Mwanaidi ambaye alikuwa akisoma Kidato cha Pili katika Shule ya Sekondari Makurumla kuuchukua mwili huo kutokana na deni walilokuwa wakidaiwa hospitalini hapo la Tsh milioni 26, kushindwa kulilipa.

 

Baada ya kuzuiliwa kwa siku tano, sasa mwili huo umekabidhiwa kwa familia ambayo ilijichangisha na kupata kiasi cha Tsh millioni tano baada ya kupewa msamaha wa zaidi ya Tsh millioni 21.8. na Ustawi wa Jamii.

 

Mama wa marehemu alisema kuwa, binti yake alikua akisumbuliwa na miguu na ndipo walipoamua kumpeleka Hospitali ya Amana.

 

Baada ya kukaa kwa muda na kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, alipewa rufaa ya kuhamishiwa Hospitali ya Mloganzila kutoka Hospitali ya Amana ambapo alitibiwa hapo hadi umauti ulipomfika.

 

TAZAMA TUKIO HILO

Comments are closed.