The House of Favourite Newspapers

LYNN: RAYVANNY DOGO JANJA WALINIPA NGUVU

Irene Godfrey Louis ‘Lyyn’

VIDEO Queen wa Bongo, Irene Godfrey Louis ‘Lyyn’ ambaye kwa sasa ameingia rasmi kwenye Bongo Fleva amefungukia waliompa nguvu kuingia kwenye muziki kuwa ni wasanii Rayvanny na Dogo Janja.  

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Lynn alisema kwa kipindi kirefu alikuwa na nia ila alikosa mtu wa kumshauri, lakini baada ya kuwasikilizisha nyimbo zake, Rayvanny na Dogo Janja walimtia moyo kuwa anaweza.

 

“Muziki ni moja ya malengo yaliyokuwa ndani yangu, lakini ndoto zangu niliona kama zinakufa kutokana na baadhi ya watu kunikatisha tamaa. “Lakini ilikuwa tofauti kwa Rayvanny na Dogo Janja ambao walinipa moyo kuwa naweza ndipo nikatoa wimbo wangu haraka,” alisema Lynn ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Diamond.

 

Lyyn ambaye ameachia ngoma inayokwenda kwa jina la Chafu na kusifia mapokezi kuwa ni mazuri kuliko alivyotegemea hivyo amepanga kuachia mwingine fasta.

Stori: Shamuma Awadhi

Comments are closed.