The House of Favourite Newspapers

Ma-Video Queen Wamechomoa Betri Mapenzi ya Watu!

0

WIVU ni kidonda na ukiushiriki utakonda, ni msemo wa Waswahili ulio na maana kubwa!

Hivi karibuni baadhi ya wapenzi wa mastaa Bongo, wamejikuta mahusiano yao yakitikisa kutokana na skendo ya waume zao kutoka na ‘ma-video vixen’.

 

Hili suala halikuanzia leo, kwani hata kipindi cha nyuma, haya mambo yalikuwepo licha ya kutopewa uzito kivile, lakini kwa kipindi cha sasa yameibuka kwa kasi hadi wengine kujiuliza, je ni kiki au ni issue ya serious?

 

Baadhi ya mastaa nchini wamejikuta wakiwa hawana maelewano mazuri kwenye uhusiano wao na wengine uhusiano wao kuvunjika kabisa kwa kile kinachodaiwa na wapenzi wao kuwa wanaume hao kutoka kimapenzi na video queen wao pindi tu wanapomaliza kurekodi video za nyimbo zao.

Hapa chini tumekuwekea baadhi ya wasanii ambapo uhusiano wao umevunjika na wengine mpaka sasa hawana uhusiano mzuri:

 

FAHYMA

Ni mwanamitindo chipukizi ambaye alijizolea umaarufu baada ya kuzaa na staa wa muziki wa Bongo Fleva kutoka kwenye lebo ya WCB, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’.

Penzi lao lilizidi kung’aa na kuwa gumzo mitandaoni baada ya kuonekana wakiambatana kila mahali, hivyo kuwafanya watu kuzidi kuwafuatilia kwa karibu.

 

Mapichapicha ya pamoja yalikuwa kama yote, huku kila mmoja akimposti mwenzake kwa mbwembwe na kuandika maneno matamu yaliyoashiria penzi zito mioyoni mwao.

 

Miaka ilivyozidi kwenda, mara paap wananzengo tukasikia wawili hao tayari wameshafunga ndoa kisiri na kinachosubiriwa kwa sasa ni kufanya sherehe tu, ambapo kuna kipindi Fahyma alivunja ukimya na kusema kwamba watafunga Desemba, 2019 lakini mwaka ukapita bila ya ndoa.

Mrembo aliyedaiwa kuchomoa betri ni Nana aliyeshiriki kwenye video ya I Love You ya Rayvanny.

 

WADAIWA KUACHANA

Hata hivyo, wakati wananzengo wakisubiri kuona ndoa, ghafla zikasambaa taarifa kuwa wawili hao wameshabwagana na baada ya kufuatilia sana ikaonekana kwamba mrembo Nanah aliyeshiriki kwenye video ya wimbo wa I Love You wa Rayvanny ndio kasababisha wanandoa hao kumwagana baada ya kudaiwa kutoka kimapenzi na msanii huyo.

 

Mbali na kwamba kila mtu alikuwa akiongea lake, lakini mwisho wa siku bibie Fahyma akaona isiwe kesi, akakubali kwamba kweli ameachana na mume wake lakini sio kwa sababu ya video queen huyo, bali kwa mambo yao binafsi lakini hivi karibuni tena ikadaiwa kuwa wamerudiana, lakini mpaka sasa hakuna ambaye yupo tayari kuthibitisha hilo.

 

TANASHA

Ni mtangazaji wa kituo cha redio cha NGR nchini Kenya, ambaye umaarufu wake ulianza kujulikana zaidi baada ya kutoka kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Urembo wake ukazidi kumvutia msanii huyo hadi kujikuta akishindwa kuzuia hisia zake na kumuweka hadharani, tofauti na alivyofanya kwa baby mama wake mwingine Hamisa Mobeto.

 

Haikuchukua muda sana mwanamama huyo akabeba ujauzito na mwisho wa siku akafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Naseeb Junior, hatujakaa sawa mara penzi lao likaanza kuingiwa na mdudu baada ya kudaiwa kumwagana huku miongoni mwa sababu zilizotajwa kuchangia penzi lao kuvunjika ni pamoja na video queen anayefahamika kwa jina la Malaika ambaye ameshiriki katika video ya Jeje ya msanii huyo.

 

Picha za Diamond na video queen huyo zilianza kusambaa mitandaoni huku kila mmoja akiongea lake, wapo waliosema Diamond ameshalala na mrembo huyo, hivyo Tanasha hana chake na wengine wakasema sio kweli bali ile ni kazi tu kama zilivyo kazi nyingine. Mpaka hivi sasa wawili hao tayari wameshaachana na mwanamama huyo amerejea nchini kwao Kenya huku Diamond akiendelea kujiita single boy.

 

SARAH

Ni mke halali wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’. Mapenzi yao yameonekana kushamiri na kupendwa na watu kwa kuwaaminisha watu kwamba hawawezi kuachana, kwani Sarah ameweza kuonekana kwenye wimbo wa Harmo wa Niteke na kuweza kuslimu ili kufunga ndoa tukufu ya Kiislam. Licha ya penzi lao kushamiri, lakini likaja kuingia shubiri ghafla.

 

Mara baada ya Harmo kutoa wimbo wake wa Bed Room, huku mwanadada mwenye umbo tata Nicole Joyberry akiwa kama video queen ndipo kisa kilipoanzia, baadhi ya watu walisema kuwa Harmo hawezi kumuacha hivihivi mrembo huyo bila ya kutoka naye kimapenzi, kwani ana mzigo wa maana.

 

Mara video ya Sarah iliyosemekana ni wakati wa kumfanyia vurugu msichana huyo ikaanza kuzagaa kwa kasi kama moto wa kifuu mitandaoni, hali iliyowapelekea wananzengo kujiuliza kuwa kumbe hata Wazungu wanaweza kufanya vurugu wakiingiliwa kwenye mahusiano yao.

Mpaka sasa penzi lao bado halipo sawa na inasemekana tayari Harmo ameshamu un-follow mwanadada huyo kwenye akaunti yake ya Instagram.

 

MAKALA | Memorise Richard na Amina Said

Leave A Reply