The House of Favourite Newspapers

Maadhimisho ya Kuchangia Damu Dar, Feb. 25-26

0

8.Daktari-wa-utoaji-damu-akimuandaa-mwanajogging-kwa-ajili-ya-kutoa-damu[1]Stori: Mwandish Wetu, Ijumaa

Dar es Salaam Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepanga kufanya Maadhimisho ya Utoaji wa Huduma ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambayo yanatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Karume (Ilala).

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza Februari 25 mpaka 26, mwaka huu kuanzia asubuhi mpaka saa 11 jioni huku yakisindikizwa na kaulimbiu ‘Changia Damu Okoa Maisha’.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo ambaye ni mmoja wa wadhamini wa ‘eventi’ hiyo amesema kwamba ni jambo zuri kwa Watanzania kujitokeza siku hizo mbili kwa ajili ya kuchangia damu na kuokoa maisha ya ndugu zetu, marafiki zetu na watu wengine.

“Ni maadhimisho mazuri, yenye lengo zuri vilevile. Nataka sisi kama Watanzania tujitokeze kwa wingi kuchangia damu kwa ajili ya watoto wetu, kaka zetu na hata dada zetu ambao wamekosa damu ya kutosha hospitalini,” alisema Shigongo.

Mbali na uchangiaji huo wa damu, pia siku hizo kutakuwa na burudani kutoka kwa kundi linalofanya vizuri hapa Bongo, Yamoto Band. Maadhimisho haya yamedhaminiwa na Hospitali ya Muhimbili, Gazeti la Championi na Kampuni ya Global Publishers.

Leave A Reply