The House of Favourite Newspapers

Maafisa Wapya wa Jeshi la Zimamoto Walioteuliwa na Rais Waapishwa

0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Operesheni Billy Mwakatage,wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.

 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonkowakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.

 

Kamishna Jenerali Thobias Andengenye, akimsikiliza Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi, akitoa utambulisho mfupi wa Makamishna wakati wa hafla fupi hiyo.

 

Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali Thobias Andengenye.

 

Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto wa Jeshi la Zimamoto na, Jesuald Ikonko, akila kiapo cha Utii.

 

Kamishna Jenerali Thobias Andengenye (watatukulia), akiwa katika picha na Kamishna wa Utawala na Fedha, Michael Shija (wapili kulia), Kamishna wa Oparesheni Billy Mwakatage (kushoto) na Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko (kulia) wakati wa hafla fupi hiyo.

 

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini Tanzania Thobias Andengenye amewaapisha maofisa wawili wa jeshi hilo walioteuliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwa mudazaidi ya miaka

 

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha amaofisa hao, ambao ni pamoja na Kamishna wa divisheni ya oparesheni Kamishna Billy Mwakatege, na Kamishna wa divisheni ya usalama wa moto kamishna Jesual Ikonko wa jeshi la zima moto, amesema wanalenga kuona huduma za uokoaji na zimamoto zikiboreshwa huku elimu ikitolewa kikamilifu kwa wananchi ya namna wanavyo weza kujikinga na majanga ya moto.

NA HILALY DAUDI | GLOBAL TV ONLINE

=====

TAZAMA VIDEO YA TUKIO LA KUAPISHWA

Leave A Reply