The House of Favourite Newspapers

Maagizo ya Waziri Mkuu kwa Wakuu wa Mikoa – Video

0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Wakuu wa Mikoa yote nchini wanapaswa kusimamia kwa karibu fedha maalum ya sh. trilioni 1.3 zilitolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kuimarisha huduma za jamii.

 

“Kule mikoani kutakuwa na kamati maalum na Mkuu wa Mkoa ndiye atakuwa Mwenyekiti wake na Katibu Tawala atakuwa Katibu wao. Pia kutakuwa na mchumi, Mhandisi wa Mkoa, Afisa Manunuzi, Afisa Elimu, Mganga Mkuu wa mkoa, Mwanasheria, Mratibu wa Sekta na tumemuongeza Mhandisi wa TARURA kwani atahitajika japo hayumo kwenye sekretarieti ya mkoa,” amesema.

 

Waziri Mkuu ametoa wito huo jana (Alhamisi, Oktoba 21, 2021) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma wakati alipokutana Mawaziri na Makatibu Wakuu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kitaifa inayosimamia miradi ya fedha za kuimarisha huduma za jamii.

 

Waziri Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, amesema Kamati za Ulinzi za Mikoa (KUU) zitakuwa na jukumu la kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo na kama kutakuwa suala rushwa wataingia na kuchukua hatua. “Katika kipindi cha miezi tisa, tunatakiwa tuwe tumekamilisha hii miradi,” amesisitiza.

Leave A Reply