Maajabu! Bibi wa Miaka 74 Ajifungua Mapacha – Video

KIKONGWE mmoja aitwaye Erramatti Mangayamma mwenye umri wa miaka 74 katika jimbo la Kusini mwa India la Andhra Pradesh jijini Guntur amejifungua watoto mapacha wawili wa kike na kuushangaza ulimwengu kwa tukio hilo la aina yake.

Mangayamma ambaye aliyejifungua Alhamisi, Septemba 6, 2019, anasemekana ndiye mwanamke wa kwanza mkongwe nchini humo kujifungua akiwa na umri mkubwa zaidi.

Bibi huyo ambaye ameishi na mumewe kwa miaka 57, hakuwahi kushika ujauzito tangu usichana wake, hali iliyomfanya kutengwa na jamii inayomzunguka na kujiona mnyonge licha ya mumewe kuendelea kuvumilia.

Wazazi waliomsaidia kujifungua mapacha hao wanasema amejifungua kwa njia ya kuanguliwa kwa mayai yake ya uzazi nje ya mfuko wa uzazi na baadaye kuchanganywa na mbegu za kiume na kisha kupandikizwa ndani ya mfuko wake wa uzazi ama IVF kwa lugha ya kitaalam.

TAZAMA MUUJIZA HUU


Loading...

Toa comment