The House of Favourite Newspapers

Maajabu ya Nyoka Mwenye Macho Matatu

MAOFISA wa wanyama pori wamesambaza picha za nyoka mwenye macho matatu aliyepatikana katikati ya barabara Kaskazini mwa Australia.

 

Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori na Bustani za Wanyama (Northern Territory Parks and Wildlife Service) wameeleza kwamba nyoka huyo ambaye picha zake zilisambaa  katika mitando ya kijamii, ni wa “kustaajabisha”.

 

Maofisa hao walimgundua nyoka huyo mwenye urefu wa inchi 15, katika mji wa Humpty Doo, 40km Kusini Mashariki mwa Darwin na kumpa jina la Monty Python lakini inaelezwa alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake.

 

Wataalamu wanasema jicho la tatu la nyoka huyo lililo juu ya kichwa chake limeonekana kuwa ni mabadiliko ya asili na baada ya uchunguzi, shirika hilo limesema picha za X-ray zimeonyesha kwamba hakuwa na vichwa viwili kwa pamoja, alikuwa na fuvu moja la kichwa na macho yote matatu yanayofanya kazi sawasawa.

 

 

Mtaalamu wa nyoka, Profesa Bryan Fry, amesema mabadiliko ya maumbile ni sehemu ya kawaida; “Kila mtoto hupitia mabadiliko ya kiwango fulani – huyu alishuhudia mabadiliko yasiyo ya kawaida,

 

“Sijaona nyoka mwenye macho matatu awali, lakini tumeona chatu mwenye vichwa viwili katika maabara yetu, ni aina tofuati ya mabadiliko kama tunavyoona kwa pacha wachanga wanaozaliwa wameungana,” alisema.

 

Hata hivyo, nyoka huyo jamii ya chatu, alifariki wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa mnamo Machi  mwaka huu.

Kweli JPM anayo KAZI! Kijana Kamueleza Alivyoombwa Rushwa ‘MHIMBILI’!

Comments are closed.